HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2017

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO


Dar es Salaam, Novemba 15.2017

Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. “Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”. alisema, Morel.

No comments:

Post a Comment

Pages