Kozi ya Grassroots kwa Vijana kuanzia miaka 6-12, itafanyika mkoani Mbeya kuanzia Novemba 27, 2017 mpaka Desemba 1, mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi
amesema kozi hiyo itahusisha walimu wa Shule za Msingi za mikoa ya
Songwe, Katavi, Rukwa na wenyeji Mbeya.
Jumla
ya washiriki 30 watahudhuria kozi hiyo ambapo kila mkoa utatoa
washiriki saba (7) isipokuwa wenyeji Mbeya ambao watatoa washiriki tisa
(9).
Kozi
hiyo imezingatia jenda kwa kila mkoa unatakiwa kutoa idadi sawa au
Wanawake wawe wengi zaidi ya Wanaume ili kutoa hamasa zaidi kwa Wanawake
kujifunza.
Kozi
hiyo ya Grassroots itakwenda sambamba na Kampeni ya ‘Live Your Goal’
ikiwa na maana ya ‘Ishi ndoto zako’ itayofanyika Novemba 29, 2017 ikiwa
na lengo la kutoa hamasa kwa soka la Wanawake.
Kampeni
hiyo ya Live Your Goal inalenga kutoa hamasa kwa wadau waujue, waupende
na kuheshimu soka la Wanawake kama ilivyo kwa upande wa Wanaume ambapo
kampeni hiyo itaambatana na shughuli mbalimbali za soka kuanzia asubuhi
na itamalizika kwa kuchezwa mchezo mmoja Uwanja wa Sokoine siku hiyo
jioni baina ya timu za Wanawake za Mkoa wa Mbeya.
Mwenyekiti
wa Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma akizungumzia kozi
hiyo kwenda kufanyika Mbeya, amesema: “Tumetoka Lindi na sasa tunakwenda
Mbeya, mpango huu utasaidia kuwajengea vijana wetu kujiamini hasa
Wanawake.”
Wakati
huohuo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias
Mwanjala amewakaribisha washiriki watakaohudhuria kozi hiyo mkoani Mbeya
akisema Mkoa huo upo tayari nkupokea ugeni huo kwa maendeleo ya mpira
wa miguu.
Mpango wa Grass roots kabla ya kwenda kufanyika Mbeya ulifanyika huko Mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment