Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID. ARUSHA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya itakayowawezesha waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kutumia mtandao wa Internet.
Mhe. Mhagama amezindua huduma hiyo leo Novemba 29, 2017, wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, Arusha.
“Huduma hii itawawezesha waajiri kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa internet na hawalazimiki kujaza fomu na kuja ofisini kwetu au kwa maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, alisema wakati akitambulisha huduma hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank plc imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni zingine zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa wafanyakazi na kampuni nyingine ni KPMG Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi wengi.
WCF iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista kwa niaba ya Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa Serikali katika kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Wadau wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi, (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshjomba, wakishuhudia Mwenyekiyti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilinhi milioni 15, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, ikiwa ni mchango wa Mfuko kusaidia mpango wa elimu mkoani humo. Makabidhiano haya yamekwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa WCF jijini Arusha.
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Bw. Richard L.Makungwa kutoka NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba.
No comments:
Post a Comment