Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma ilipowasili kukagua kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.
KIGOMA , Tanzania
Takribani raia 800 kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekimbilia Nchini Tanzania kuomba hifadhi
ya ukimbizi katika kijiji cha Kigadye Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma wakihofia
machafuko.
Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu
kusini mwa Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na
vikundi mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu
na hivyo kuanza kukimbia nchini Tanzania
kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Wakizungumza mbele ya kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyotembelea katika kituo cha kupokelea
waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia hao walisema sababu iliyowafanya
kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa maisha yao kutokana na mapigano
yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na Serikali iliyopo madarakani.
Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma Brigedia Jenerali (mst.) Emannuel Maganga akiongoza kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika kuwaona raia hao na wanafana
jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma muimu za kibinadamu zinaboresha
katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa
kuwasikiiza raia hao.
Kutokakana na wimbi kubwa hilo
huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi zinahitajika haraka ili kuwahudumia
raia hao ambao wengi wao ni kinamama na watoto.
Baadhi ya raia waliokimbilia
nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na kuahirishwa Uchaguzi Mkuu uliopaswa
kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka kwa mzozo wa mapigano uenda ukawaathiri
amani nchini Congo, Vyama vya upinzanu
vimeanza kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi, wamehofia amani.
Kituo cha kigadye wilayani
kasulu, huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia wa Congo wanaoendelea
kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini mwao. Kusini mwa Congo
kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio ya mara kwa mara yanayosabisha
hofu ya machafuko kwa wananchi.
Habari na Picha zimeandaliwa na.
Gabriel
Ng’honoli
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
No comments:
Post a Comment