SERIKALI imesaini mikataba minne na kampuni nne za ujenzi wa barabara
yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 702 kwa ujenzi wa kilomita 402.
Tukio
hilo kusaini mkataba hiyo limeshughudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwakilishi Makazi wa Benki ya
Mandeleo Afrika (ADB), Hellen Minja, wabunge ambao barabara zitajenfwa,
wawakilishi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na wakandarasi
walioshinda zabuni.
Akizungumzia
utiaji saini huo Waziri Mbarawa alisema fedha hizo zitatumika katika
ujenzi wa barabara kutoka Tabora, Usesula hadi Mpanda Katavi kilomita
335 na kilomita 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Mbarawa
alisema ujenzi wa barabara hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), na ahadi za Rais John Magufuli wakati wa kampeni.
Alisema
fedha hizo zimetolewa na ADB ikiwa ni baada ya serikali kuomba msaada
mwaka 2015 ili kuweza kufungua fursa zilizopo katika maeneo husika kwa
miradi.
Waziri alitumia
nafasi hiyo kuwataka wakandarasi walioshinda zabuni kujenga barabara
zenye ubora na viwango kwa kuzingatia muda wa ujenzi.
Mbarawa alisema nia ya serikali ni kuona ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
"Naomba
Tanroads msimamie ujenzi wa barabara yenye ubora kwani wakandarasi
wengi ni wajanja na ikitokea mtu ameharibu asipewe nafasi kabisa ya
ujenzi wa barabara hapa nchini," alisema.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale alisema
wakandarasi waliopewa kazi wametokana na uchambuzi mkubwa uliofanyika
kati ya wakandarasi 129 waliojitokeza mwaka 2016.
Alisema
ili kurahisisha ujenzi wa barabara hizo wamegawa kwa wakandarasi wanne
ambapo barabara ya Usesula hadi Komanga kilomita 108 itajengwa na
Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Group Corporation Limited ya China
kwa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni 158 na itajengwa kwa miezi 36.
"Komanga
hadi Kasinde kilomita 108 itajengwa na Mkandarasi Kampuni ya China Wu
Yi Co. Limited kwa zaidi ya sh.billioni 140 na Kasinde hadi Mpanda
kilomita 105 Mkandarasi Kampuni ya China Railway Seventh Group Co.Ltd
kwa sh. Bilioni 133," alisema.
Mfugale
alisema barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay kilomita 67 inajengwa na
Mkandarasi China Henan International Corporation Group Co.Ltd (Chico)
kwa sh. Bilioni 129.
Alisema Tanroads imejipanga kusimamia ujenzi huo kwa kufuata viwango vinavyohitajika vya ujenzi wa barabara nchini.
Mwakilishi
Mkazi wa ADB, Minja alisema ofisi yake itaendelea kutoa mchango kwa
serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini pale watakapo
hitajika.
Minja alisema matarajio ya ADB nikuona Tanzania inapata maendeleo kwa haraka na njia rahisi ni kupitia miundombinu.
Waziri
wa Majj na Umwagiliaji Mhandisi Azack Kamwele ambaye barabara ya Tabora
hadi Mpanda inapita jimboni kwake alisema ujenzi huo utafungua fursa
mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji alisema barabara
hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania, Msumbiji na Malawi.
Alisema Nyasa ina vivutio vingi vya utalii hivyo ujio wa barabara hizo utakuwa njia rahisi ya kuwafikisha watalii eneo hilo.
No comments:
Post a Comment