Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Samwel Wangwe (wa
pili kushoto), akipata maelezo kuhusu mbegu ya mkonge kutoka kwa Meneja Mkuu wa
Mkonge Energy Systems, Gilead Kissaka, wakati wajumbe wa bodi hiyo walipotembelea
shamba la mkonge la Hale Korogwe mkoani Tanga, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Katani, Salum Shamte. (Picha na Francis Dande).
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa NSSF, Justine Mwandu, akimwagilia maji mti alioupanda kama kumbukumbu ya bodi hiyo ilipotembelea miradi ya uwekezaji mkoani Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akipanda mti wa kumbukumbu ya Bodi ya Udhamini wa NSSF ilipotembelea miradi ya uwekezaji mkoani Tanga.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Magreth Chacha akipanda mti wa kumbukumbu.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Kampuni ya Katani, Juma Shamte akipanda mti.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa
NSSF, Justine Mwandu (katikati), wakiangalia utayarishaji wa kamba za katani wakati
wajumbe wa bodi walipotembelea Kiwanda cha kusindika mkonge cha Magoma-kulasi
kilichopo Korogwe vijijini mkoani Tanga, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Katani, Salum Shamte.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara (katikati), akiangali singa za mkonge walipotembelea Kiwanda cha kusindika mkonge cha Magoma-kulasi
kilichopo Korogwe vijijini mkoani Tanga, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Katani, Salum Shamte.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Prof. Samwel Wangwe akipanda mmea wa Mkonge.
Meneja Mkuu wa
Mkonge Energy Systems, Gilead Kissaka, akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa NSSF kuhusu shamba la mkonge la Hale Tanga.
Wajumbe wa bodi wakipata maelezo walipotembelea kiwanda cha Umeme Mkonge.
Wajumbe wa Bodi wakitembelea kiwanda cha Umeme Mkonge.
Ufafanuzi.
Meneja Mkuu wa
Mkonge Energy Systems, Gilead Kissaka, akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya udhamini wa NSSF walipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Umeme unaotumika kwa ajili ya matumizi ya kiwanda cha kuzalisha bidhaa zitokanazo na mmea wa mkonge.
Picha ya pamoja baada ya kutembelea kiwanda cha Umeme Mkonge.
Picha ya pamoja.
Wajumbe wa Biodi ya Udhamini wa NSSF wakiangalia hatua mbalimbali za utengenezaji wa kamba za mkonge.
Sehemu ya utengenezaji wa mazulia ya mkonge.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (kushoto), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Samwel Wangwe (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Katani, Salum Shamte (kulia).
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Justine Mwandu (kulia) akiangali bidhaa zinazotokana na mkonge.
Meneja Udhibitti Ubora wa Kiwanda cha Tancord, John Mtemi (katikati), akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa NSSF walipotembelea kiwanda hicho.
Meneja
Udhibitti Ubora wa Kiwanda cha Tancord, John Mtemi (katikati), akitoa
maelezo kuhusu ubora wa kamba za mkonge.
No comments:
Post a Comment