Droo ya raundi ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho
la Azam (ASFC) inachezeshwa kesho Januari 5, 2018 ikishirikisha timu 32.
Raundi hiyo ya Tatu itahusisha timu nne(4) za
mabingwa wa mikoa timu tatu(3) za Ligi Daraja la Pili,timu Kumi na Mbili
(12) za Ligi Daraja la Kwanza na timu 13 za Ligi Kuu.
MAAMUZI KAMATI YA MASHINDANO
Kikao cha kamati ya Mashindano kilichokutana
Desemba 29, 2017 kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kujadili mchezo namba 31 na 32 uliohusisha timu za Abajalo FC dhidi ya
Tanzania Prisons ya Mbeya na ule kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu katika Kombe la
Shirikisho la Azam (ASFC) iliyokuwa ifanyike Desemba 20, 2017 kwenye Uwanja wa
Uhuru na Chamazi.
Kamati ilikaa na kupitia taarifa mbalimbali za
michezo hiyo.
MAAMUZI KAMATI YA NIDHAMU
Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia
ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa
Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City
uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA(TFF)
No comments:
Post a Comment