January 04, 2018

MPIGAPICHA TSN KUZIKWA LEO

Mwili wa aliyekuwa mpigapicha wa gazeti la Habari Leo, Athumani Hamisi Msengi unataraji kuzikwa hapo kesho Januari 5, 2018 baada ya Swala ya Ijumaa na Maziko yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Sinza Madukani  Mtaa wa Weruweru (Njia ya Namnani Hotel Nyumba na 26).

Marehemu Athumani Hamisi amefariki asubuhi ya leo Januari 4,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake, Marehemu ameacha familia yenye watoto watano.

TUNATOA POLE KWA WOTE MLIOFIKWA NA MSIBA HUU.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa mpigapicha wa gazeti la Habari Leo, marehemu Athumani Hamisi nyumbani kwake Sinza jijini.
 Baadhi ya ndugu wakiwa msibani.
Waombolezaji.

No comments:

Post a Comment

Pages