Wateja watatu wa Tigo
Pesa wapokea TZS 15 milioni, 10 millioni na 5 milioni kila mmoja.
- 12 wengine washinda TZS milioni moja (1) na wengine 49 wapata TSH 500,000 kila mmoja katika kilele cha promosheni
Dar es Salaam, 5 Januari, 2018.
Tigo Tanzania, kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, leo imegeuza Watanzania watatu (3) kuwa
mamilionea kupitia promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’
iliyofikia tamati usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva
na mkaazi wa Mbezi Makonde, Dar es Salaam leo amepokea donge nono la
shilingi 15 milioni kutoka Tigo. ‘Sasa
nina rasilimali itakayoniwezesha kufanikisha malengo yangu ya kufanya kilimo mwaka
huu,’ alisema.
Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi
wa Tunduru, Ruvuma naye alishinda shilingi milioni kumi (10) baada
ya kutumia huduma ya Tigo Pesa katika kipindi cha msimu wa sikukuu na mwaka
mpya. ‘Nilikuwa nimeshalala wakati nilipokea simu kutoka Tigo iliyonifahamisha
kuwa nimeshinda mamilioni ya shilingi. Nilidhani kuwa ni ndoto na asubuhi
nilipoamka nikawapigia Tigo simu kuhakikisha taarifa hizi na kugundua kuwa ni
za kweli. Nimeanza mwaka mpya kwa nguvu mpya!’ alisema.
Naye Mariam
Josef Maligisa kutoka Nagangu mkoani Lindi alisema kuwa maisha yake
kama mkulima na mfanya biashara ndogo yataboreshwa kwa kiasi kikubwa na zawadi
ya shilingi milioni tano (5) kutoka Tigo. ‘Sikuwa na nyenzo za kilimo
ila sasa nitaweza kuongeza eneo ninalolima pamoja na kukuza biashara yangu,’
aliongeza.
Washindi wengine
12 walinyakua zawadi za shilingi milioni moja (1) kila mmoja huku wengine 49
wakijipatia zawadi za shilingi laki tano (500,000/-) kila mmoja kama zawadi za
kila siku.
Akikabidhi zawadi
kwa washindi katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Wateja wa
Tigo Pesa, Mary Rutta alielezea
furaha yake kuwa promosheni hiyo imefanikiwa kuboresha maisha ya wateja wa Tigo
Pesa.
‘Tumefikia lengo kuu la promosheni hii ambalo lilikuwa
ni kufanikisha ndoto za wateja wetu katika kipindi cha sikukuu na mwaka
mpya.
Alibainisha kuwa
katika promosheni hiyo, Tigo imetoa
jumla ya TZS 120 milioni kama zawadi kwa washindi 153 tofauti kutoka maeneo
tofauti ya nchi, ambapo wateja walipata fursa ya kushinda baada ya kufanya
miamala kupitia Tigo Pesa katika kipindi cha sikukuu na mwaka mpya.
‘Pia
tunajivunia mchango wetu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa
watu wote nchini. Tigo Pesa inawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma,
kupokea na kufanya miamala ya fedha inayofikia zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi. Huu ni mchango mkubwa
kwa uchumi wa watu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla. Tigo Pesa ni zaidi ya
huduma ya kutuma na kupokea fedha. Ni sehemu ya maisha,’ aliongeza.
Tigo Pesa ndio huduma ya pili kwa ukubwa nchini
ya huduma za pesa kwa njia ya simu za mkononi, inayojivunia mtandao mpana wa
mawakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.
Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya
kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya
kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia
inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.
No comments:
Post a Comment