JAJI MKUU wa Zanzibar, Omar Othman Makungu,
Katika amewataka, mahakimu wasifanye
kazi kwa mashindikizo ya wanasiasa, kwani wakifanya hivyo watakuwa hawaitendei haki
fani yao.
Jaji huyo alieleza hayo kwa nyakati
tofauti, alipokuwa akizungumza na watendaji wa mahakama za mwanzo Wingwi, Konde
na Wete, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba.
Alieleza
kuwa umefika muda Mahakimu wafanye kazi zao kisayansi na kuacha mashindikizo
ambayo yataharibu uwaminifu wao kwa jamii.
“Lazima muelewa mahakimu wetu kwamba, kuna
kupanda daraja kwa mujibu wa kazi zenu, lakini kama mnafanyakazia kwa chuki,
mashindikizo basi msitarajie kupanda ngazi,”alieleza Jaji Makungu.
Sambamba na hilo aliwauliza mahakimu kisiwani
humo, wamezitoa wapi sheria zinazowapa mamlaka ya kuwalazimisha watuhumiwa kuwa
na wafanyakazi wa serikali au barua za masheha wanapoomba dhamana dhidi ya kesi
zinazowakabili.
Alisema anashangaa kuona baadhi ya mahakimu hao, kuwawekea masharti magumu watuhumiwa, kwa lengo la kutafuta sababu ya kuwapelekea rumande, jambo ambalo sio sahihi maana huko sio kwahali kwema kwa kukaa mwanadamu.
Alisema lazima mahakimu wafahamu kuwa, kumpeleka mtuhumiwa rumande ni hatua ya mwisho, na sio iwe ndio kipaumbele chao, kwa kuwekea masharti magumu au kima kikubwa cha fedha.
Alieleza kuwa, yeye binafsi hajaona popote kwenye sheria, kuwa mtuhumiwa
anatakiwa ili kutimiza masharti kwambaawe na mtu anaefanyakazi serikalini, au
barua ya sheha kwamba ndio kigezo namtuhumiwa akishindwa na hayo, apelekwe
rumade.
“Jamani wale ni binadamu, wapo waliotenda makosa, wapo walioteleza nawengine wamesingiziwa sasa na nyinyi mkishawishika kwa kuwapeleka rumade, tena kwa mashartimazgumu,mtakuwa mtakuwa hamukuwatendea haki” alieleza jaji Makung
Nae Mrajisi wa jimbo mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein, alisema changamoto kadhaa wamezisikia hawa walipowatembelea wanafunzi,
juu ya kucheleweshea mienendo ya kesi, jambo kwa sasa wanajitahidi kuliepuka.
Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar akiwa na Mrajisi na Manaibu Warajisi, itaendelea tena kesho kwa kulikagua jengo la Mahakama Kuu Chakechakeya kuzungumza na watendaji wake, na kukamilisha ziara yake ya Siku Nne kisiwani humo.
No comments:
Post a Comment