WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za
miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika
Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Ameyasema hayo leo (Jumanne,
Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye
Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.
Waziri
Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka
Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na
Jeshi la Magereza.
“Nimeridhika
na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha
maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka
maeneo mbalimbali.”
Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia
kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar,
chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh
Abeid Aman Karume.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
S. L.
P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMANNE,
APRILI 24, 2018.
No comments:
Post a Comment