May 18, 2018

DONGOBESH FC YAICHAPA STAND FC YA HAYDOM GOLI 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KURUGENZI CUP 2018

 Mchezaji wa timu ya Dongobesh FC Antipas Vicent akiwa amebebwa juu juu na mchezaji mwenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika yake na timu ya Stand FC ya Mjini Haydom ambapo mchezaji huyo ndiye aliyeifungia timu yake goli 1-0 na timu ya Dongobeshi kufanikiwa kuingia nusu fainali katika michuano ya Kurugenzi Cup 2018 linaloandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.ikidhaminiwa na Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha Iringa.
 Wachezaji wa timu ya Dongobash FC wakisikiliza maelezo ya Mmoja wa Waratibu wa michuano hiyo Bw. Phars Nyanda wakati akiwapa utaratibu mara baada ya mchezo huo kumalizika.
 Benchi la Ufundi la Timu ya Dongobesh FC likinyanyuka juu na kushangilia mara baada ya kuifunga timu ya Stand FC ya mjini Haydom katika mchezo uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.
 Golikipa wa timu ya Stand FC ya mjini Haydom akisaidiwa na wenzake mara baada ya kuumia wakati wakiwania mpira uliokuwa unaingia golini mwake katika mchezo huo.
 Hekaheka golini mwa timu ya Stand FC ya mjini Haydom wakati wachezaji wa timu ya Dongobesh FC wakiliandama goli la wapinzani wao.
 Picha zikionyesha wachezaji wa Dongobesh FC na Stand FC ya Haydom wakichuana kuwania mpira wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Shule ya msingi Haydom leo.
 Picha zikionyesha wachezaji wa Dongobesh FC na Stand FC ya Haydom wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliofanyika  kwenye uwanja wa Shule ya msingi Haydom leo.

 Kikosi cha timu ya Dongobesh FC kilichotinga Fainali baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Stand FC ya Haydom.
 Kikosi cha timu ya Stand FC ya Mjini Haydom kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo
 Picha mbalimbali zikionyesha mashabiki wa soka wa mjini Haydom walivyojitokeza kushuhudia mchezo huo.
 Akina mama ni miongoni mwa mashabiki wa soka wa mjini Haydom waliojitokeza kushuhudia mchezo kati ya Stand FC ya mjini Haydom na Dongobeshi FC.

No comments:

Post a Comment

Pages