June 18, 2018

GERALD MWANILWA AIBUKA MSHINDI KAMPENI YA BENKI YA CRDB YA SHUHUDIA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2018 NA TEMBOCARDVISA

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi tiketi yake mshindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa wiki ya sita, Gerald Mwanilwa.
Mshindi wa wiki ya sita wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa na TemboCardVisa, Gerald Mwanilwa, akitoa neno la shukrani baada ya kupokea tiketi ya kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi mshindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa, Gerlad  Mwanilwa, Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia), akifafanua jambo kuhusu utaratibu wa kusafiri mshindi wa wiki ya sita wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa na TemboCardVisa, Gerald Mwanilwa (kushoto). 

No comments:

Post a Comment

Pages