June 17, 2018

MSHINDI WA KAMPENI YA 'SHUHUDIA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2018 NA TEMBOCARDVISA AKWEA PIPA KWENDA URUSI

Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’, Mohamed Kinjenge (katikati), akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki huku akiambatana na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kulia), pamoja na maofisa wengine wa Benki ya CRDB muda mfupi kabla ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia.

Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’, Mohamed Kinjenge (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (wa pili kushoto), akizungumza na mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa’, Mohamed Kinjenge, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, kabla ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia. Wengine wanaoshuhudia ni maofisa wa benki ya CRDB.

Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’, Mohamed Kinjenge (katikati), akitoa neno la kushukuru.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (wa pili kushoto), akiagana na mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa’, Mohamed Kinjenge, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, kabla ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia. Wengine wanaoshuhudia ni maofisa wa benki ya CRDB.

Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa’, Mohamed Kinjenge (kulia), akisindikizwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto), wakati akielekea nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa’, Mohamed Kinjenge, akifurahia safari yake ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018.

Kutoka kushoto ni Meneja Huduma za Kibenki kwa Njia ya Kielektroniki, Mangire Kibanda, Ofisa Masoko, Florence Mboli, Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Willy Kamwela na Mohamed Kinjenge ambaye ndiye mshindi wa Wiki ya Kwanza.
Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa’ Mohamed Kinjenge (kulia), akiwapungia mkono maofisa wa Benki ya CRDB (hawapo pichani), waliomsindikiza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati akielekea nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018. Kushoto ni Meneja Huduma za Kibenki kwa Njia ya Kielektroniki, Mangire Kibanda ambaye anaambatana na mshindi huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages