June 05, 2018

I&MBANK YAFUTURISHA WATEJA WA MKOA WA DAR ES SALAAM

I&MBank imeandaa futari Maalum kwa ajili ya wateja wake wa Dar es Salaam katika kuadhimisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa futari hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa I&M Bank, Baseer Mohamed, amesema kuwa anawashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wa kibiashara ambao umeifanya benki hiyo kuendelea kusimama vyema.

'Mwezi wa Ramadhani unajulikana kama moja ya kati ya nguzo za Dini ya Kislamu na Benki ya I&M kwa kutambua umuhimu wake katika Jamii imeandaa futari hii kama sehemu ya matendo yanayopaswa kufanywa na wanajamii katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani' Amesema Baseer.

'Benki yetu itaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibishara wa mwaka 2018 na kuhakikisha kuwa inaendelea kupata ukuaji endelevu kutokana na tumejipanga kuanzisha huduma mpya ya pamoja na kutanua wigo wetu wa utoaji huduma kupitia njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki' alisema Baseer.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed akizungumza na Wateja wa benki hiyo waliofika katika futari iliyoandaliwa na Benki yake katika Mwezi hu Mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya Maofisa wa I&MBank wakipata futari.

Mkurugenzi wa bodi ya I&MBank, Alan Mchaki, akitoa neno la Shukrani kwa wateja waliofika katika futari hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa I&MBank, Ndabu Swere akizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma za benki hiyo katika kipindi cha mwak 2018.
Meneja Masoko naUhusiano wa I&MBank, Emmanuel Kiondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

Sehemu ya Wateja wa Benki ya I&M Wakifuatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo.

Wateja wadau mbalimbali wa I&MBank wakipata futari.

Wadau na wateja wa I&MBank wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Wakati wa kupata futari.

Wateja wakipata fuatari.

Sehemu ya Wafanyakazi wa I&MBank wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya futari katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages