June 20, 2018

PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUONA UTENDAJI KAZI WA MFUMO UNGANISHI WA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA ARDHI (ILMIS)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Makazi Dk. Moses Kusiluka, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora, walipotembelea chumba kinachoandaa majalada ya Msajili wa ardhi kwa kupitia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) katika Ofisi hiyo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam. 
Msimamizi  wa Mradi Erick Gies Kisai akimweleza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora namna chumba hicho kinavyoendesha kazi za usajili wa ardhi katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu  Prof. Faustin Kamuzora akisisitiza jambo baada ya kutembelea chumba kinachoanda Majadala ya usajili wa ardhi kupitia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi ( ILMIS) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Ofisi za Wizara ya Ardhi tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi  katika chumba cha uandikishaji wa ardhi ngazi ya kamishna wakiendelea na kazi wakati Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea mradi huo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi  Uandikishaji wa Ardhi ngazi ya Kamishna Costa Chaula akimwelezea Prof. Faustin Kamuzora namna wanavyofanyakazi katika chumba hicho wakati wa ziara fupi iliyofanywa ofisini hapo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam. 
Prof. Faustin Kamuzora akiuliza jambo wakati alipotembelea chumba kinachohusika na uandaaji wa mifumo ya uandikishaji ardhi katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi na Makazi tarehe 20 Juni, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Mifumo ya Tehama Lameck Kafunzile  akimwelezea Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora namna mitambo iliyoo katika  chumba hicho inavyofanyika katika kuendesha shughuli za Tehama kuendesha Mfumo Unganishi wa Usimaizi wa taarifa za Ardhi (ILMIS)
Prof. Faustine Kamuzora asisitiza jambo baada ya kupata maelezo ya namna chumba cha uendeshaji wa mitambo ya Tehama kinavyofanyakazi wakati wa ziara fupi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Ardhi tarehe 20 Juni,2018 Dar es Salaam.  
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora amefurahishwa na utendajikazi wa Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia uliopo katika Wizara ya Ardhi jijini Dar es Salaam.
Mradi huu utasaidia kupatikana kwa taarifa kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa utunzaji wa taarifa za wananchi na kupunguza muda wa kutafuta taarifa kama ilivyokuwa hapo awali, alisema Prof. Kamuzora.

“Mfumo huu pia utaiwezesha Serikali kutambua walipajiwa wa ardhi, itasaidia kuboresha mazingira mazuri ya kufanya biashara na vilevile ukusanyaji wa mapato utaongezeka kwa wingi ambapo kwa sasa Mradi huu unatekelezwa katika wilaya mbili za mfano Kinondoni na Ubungo”. Alisema Prof. Kamuzora.

Serikali imejipanga kuongeza wataalamu watakaoweza kuendesha mifumo hii pale wafadhili watakapoukabidhi ili tuumiliki na tuwezwe kuendeleza na hata kwenda kwenye mikoa mingine ili kuweza kutoa huduma za kisasa kwa wananchi.

Mapema: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dr. Moses Kusiluka alisema, serikali imetenga fedha ili kuweza kuwajengea uwezo wataalamu wa Tehama ili kuwezo kutumia mfumo huo pale wafadhili watakapo ukabidhi rasmi katika Wizara ya Ardhi.

Imetolewa na
 
Afisa Habari
 
Ofisi ya Waziri Mkuu
Juni 20,2018

No comments:

Post a Comment

Pages