June 10, 2018

KONGAMANO KUHUSU UMUHIMU WA ONGEZEKO LA LIKIZO YA UZAZI KWA WAZAZI WA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA WAKATI 'NJITI' LAFANYIKA DAR

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza jambo wakati wa mjadala uliohusu umuhimu wa ongezeko la likizo ya uzazi kwa wazazi wenye watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti), uliyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dae r es salaam mwishoni mwa wiki. wengine pichani kutoka kulia ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe, Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ahmad Makuwani pamoja na Mdau wa maswala ya Watoto Njiti, Innocent Mungy.
 Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe akichangia mada ya umuhimu wa ongezeko la likizo ya uzazi kwa wazazi wenye watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti), liyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation) katika warsha ya siku moja iliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dae r es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Pages