Dar es Salaam, Tanzania
Tigo Pesa, Huduma ya Kifedha ya Kampuni ya Tigo Tanzania, imezindua kampeni ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’, kama uthibitisho kuwa huduma hiyo sasa ina hadhi ya huduma kamili ya kifedha ambayo inawapa wateja huduma za kipekee, bora na nyingi zaidi kupitia mtandao wa simu.
‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’ inazingatia
sifa ya Tigo kuwa mtandao pekee unaobuni huduma na bidhaa kulingana na mahitaji
ya wateja ili kuboresha na kurahisisha maisha yao.
‘Tigo
Pesa imepanua wigo wa bidhaa na huduma zake na kuibua njia bora zaidi kwa
wateja kufurahia huduma za haraka, uhakika na salama za kifedha popote walipo
nchini Tanzania,’ Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo aliwaambia
waandishi wa habari.
Kama
sehemu ya kampeni hii, Tigo Pesa inajivunia kuwa mtandao pekee na wa kwanza wa
simu unaotoa huduma inayowezesha wateja wa Tigo kurudisha miamala ya fedha zilizotumwa
kimakosa kwenda kwa wateja wenzao wa Tigo.
Huduma hiyo inayopatikana kupitia menu ya Tigo Pesa *150*01# inawapa wateja wa Tigo uwezo wa kurudisha
kwa haraka miamala yoyote ya kutuma hela ikiwa watagundua kuwa wamekosea
miamala hiyo, bila ya kuhitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha
huduma kwa wateja.
‘Huduma
hii ya kipekee ya kurudisha miamala iliyokosewa kwa haraka inajibu mahitaji ya
wateja wengi ambao kwa sababu moja au nyingine wanafanya makosa pindi wanapotuma
pesa. Ni huduma ya aina yake ambayo inawapa wateja uwezo zaidi juu ya miamala
wanayofanya na imeundwa kwa kuzingatia vigezo vya hali ya juu vitakavyozuia
matumizi mabaya ya huduma hii,’ Hussein alifafanua
Hivi karibuni, Tigo Pesa ilifungua ukurasa mpya wa
maisha yasiyotegemea pesa taslim nchini, baada ya kuwa kampuni ya simu ya
kwanza na pekee kuzindua huduma ya Tigo Pesa Masterpass QR.
Huduma hii inawezesha wateja kulipia huduma na bidhaa haraka, kwa urahisi na
usalama zaidi kwa njia ya kuscani nembo ya Masterpass Quick Response inayopatikiana
katika maeneo tofauti ya manunuzi/huduma.
Tigo
pia imeingia katika ushirikiano wa kipekee na kampuni ya teknologia ya Uber
yanayowezesha wateja wa Tigo kutumia huduma za usafiri za Uber kwa bei ya
punguzo na bila gharama za data. Ushirikiano huu ni muhimu kwa madereva na
wasafiri wa Uber kwani unawezesha wateja zaidi kutumia Uber App kupitia simu
zao na kupata usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi na kwa bei
ya punguzo. Kupitia Tigo Pesa pekee, wateja wa Tigo pia wana fursa ya kupata
usafiri wa Uber bure kila mara wanapofanya miamala ya fedha kati ya akaunti zao
za benki na akaunti zao za Tigo pesa.
Tigo Pesa ndio huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao
inayokuwa kwa kasi zaidi nchini, ikiwa na wateja waliosajiliwa zaidi ya milioni
saba, mtandao wa waanya biashara (merchants) zaidi ya 40,000 na mawakala zaidi
ya 85,000 walioenea kote nchini.
Tigo ndio kampuni inayoongoza maisha ya kidigitali katika
soko la mawasiliano ya simu nchini kwa miaka mingi. Tigo Pesa ndio huduma ya
kwanza ya fedha kutoa gawio la faida kwa wateja wake. Tigo pia iliongoza juhudi
za kuunganisha mitandao ya simu na mabenki ili kuunda mfumo wa kwanza duniani wa
kifedha baina ya mabenki na mitandao ya simu. Mfumo huu umeongeza idadi ya
miamala pamoja na kukuza ongezeko la idadi ya watu wanaotumia huduma rasmi za
kifedha nchini. Tigo pia ilikuwa kampuni
ya kwanza ya simu za mkononi nchini na Afrika Mashariki kutoa huduma inayowezesha
wateja kutuma na kupokea pesa kutoka nchi moja hadi nyingine kwa thamani ya sarafu
ya nchi husika, hivyo kurahisisha na kuongeza wigo wa huduma za uhamishaji
fedha baina ya nchi.
‘Kupitia kampeni ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’, Tigo inawaalika kutathmini hatua kubwa
ambazo Tigo pesa imepiga katika kipindi hiki cha miaka michache. Kampeni hii
pia inamkaribisha kila mtu kujiunga katika safari hii ya kipekee itakayowawezesha
wananchi na biashara nyingi zaidi kuongeza idadi ya wanaotumia huduma rasmi za
kifedha, kuboresha mazingira ya kidigitali na kufungua ukurasa upya wa maisha
yasiyotegemea pesa taslim,’’ Hussein alibainisha.
No comments:
Post a Comment