Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
akiangalia zao la mahindi katika shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu Arusha
leo Agosti 3, 2018 alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi.
Shamba hilo linaukubwa wa hekari 150 na limelimwa katika msimu wa Kilimo mwaka
2017/2018. Matarajio ya mavuno ni zaidi ya gunia 2,500 yenye ujazo wa kilo 90(kushoto)
ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
Anderson Kamtiaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike(wa pili toka kushoto) akikagua shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu
Arusha leo Agosti 3, 2018 kama inavyoonekana katika picha.
Bwana Shamba wa Gereza Kuu Arusha, Mkaguzi Msaidizi
wa Magereza, Ayub Mahai(wa pili toka kulia) akitoa maelezo ya kitaalam mbele ya
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini kuhusiana na uzalishaji wa zao hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike akiangalia zao la maharage yaliyolimwa msimu wa Kilimo mwaka 2017/2018
na kuvunwa mapema mwezi Julai mwaka huu, kwa sasa yapo katika hatua ya
upepetaji na kuhifadhiwa kwa chakula cha wafungwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
akimsikiliza Mkuu wa Oparesheni Maalum
katika Gereza Kuu Arusha, Mkaguzi wa Magereza, Francis Tabu alipotembelea
Gereza hilo leo Agosti 3, 2018. Kamishna Jenerali Kasike amezunguza na Maafisa
na askari wa Jeshi hilo ambao wanatekeleza majukumu ya Oparesheni Maalum katika
magereza ya Mkoa wa Arusha.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na askari kutoka
Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza leo Agosti 3, 2018 alipotembelea Gereza Kuu
Arusha(Picha zote na
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

No comments:
Post a Comment