WAZIRI MKUUKassim Majaliwa
amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90
baada ya Serikali kufanikiwa kudhibiti biashara hiyo.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 17, 2018) baada ya kufungua mkutano
wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi
za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC),
unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika unatarajiwa
kutoka na maazimio ya namna ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya
katika mataifa hizo.
Waziri
Mkuu amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga
mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya
dawa za kulevya katika nchi hizo.
“Ni
lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji
na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu
kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana
na uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa
kwa kuchanganywa na mazao ya chakula.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa
matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011.
Amesema
hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu
vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina
ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yameathiri sekta
mbalimbali ikiwemo ya afya, uchumi na jamii, uchunguzi umebainisha kuwa
kati ya asimilia 20 hadi 50 ya watumiaji wanamaambuzi ya ugonjwa wa
ukimwi.
Amesema
ni muhimu kwa nchi zote kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kisheria
ya kimataifa katika udhibiti wa biashara za dawa za kulevya, ambao
hutegemea mikataba yote ya msingi ya Umoja wa Mataifa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 17, 2018.
No comments:
Post a Comment