HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2018

Mzumbe yawaunganisha wanataaluma, wakurugenzi

Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe (Taaluma), Prof. Ganka Nyamsogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa la Biashara na Menejimenti katika nchi zinazoendelea lililofanyika jijini Dar es Salaam. 



Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akizungumza katika kongamano hilo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma, Profesa Ganka Nyamsogoro,akitoa hotuba yake wakati kongamano la Kimataifa la Biashara na Menejimenti katika nchi zinazoendelea lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma, Profesa Ganka Nyamsogoro,akitoa hotuba yake wakati kongamano la Kimataifa la Biashara na Menejimenti katika nchi zinazoendelea lililofanyika jijini Dar es Salaam.







Mkuu wa Shule ya Biashara Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Hawa Tundui, akizungumza katika kongamano hilo.
 
Na Mwandishi Wetu


CHUO Kikuu Mzumbe kimezindua jukwaa linalowaunganisha wanataaluma na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwenye jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Biashara na Utawala kwa Masoko yanayoibukia, Mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi, alisema lengo ni kutafuta namna mbadala ya kupata fedha kwa ajili ya wajasiriamali wadogo.

“Vijana wajasiriamali wanaoibukia hawana vigezo vya kukopa benki maana wanakuwa wanaanza biashara wengi hawana mali zisizohamishika na mitaji yao ni midogo, hivyo tunashirikiana na wanataaluma kutoka nchi mbalimbali ili kuona njia bora ya kupata fedha zitakazokuwa kwenye mfuko wa pamoja.

“Tunajadili pia namna ya kuwafundisha wanafunzi wawe wajasiriamali kwenye uchumi wa viwanda, tunaboresha mitaala yetu ndio maana tumezindua jukwaa, linalowahusisha watendaji wakuu wa makampuni na wasomi.

“Jukwaa hili ni muhimu kusema kweli vyuo vikuu havitakiwi kujitenga na kinachotokea kwenye ulimwengu wa kazi… tunapotengeneza mitaala yetu iendane na soko tusitengeneze kwa sababu tunajua vitu bali soko linahitaji nini.

“Ndio maana kunakitu kizuri kimekuja, Mkuu wetu wa Chuo, Profesa Lugano Kusiluka, alituzungumzia, ni kuwepo haja ya sisi walumu twende viwandani tuvione kusudi unapokuja kuzungumzia uchumi wa viwanda uwe umekiona kiwanda chenyewe na kinavyofanyakazi.

“Tunataka kutengeneza mitaala itakayotatua changamoto za ajira ndio maana tunaihuisha mitaala yetu ili wenye makampuni na wafanyabiashara wawe wanakuja vyuoni kueleza kwa vitendo wakati sisi tunawafundisha kwa nadharia kuhusu uchumi wa viwanda, wao wawaoneshe kwa vitendo.

Akizungumzia kongamano hilo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma, Profesa Ganka Nyamsogoro, alisema wanataaluma kutoka nchi mbalimbali wameunganisha nguvu ili kuona mchango wa wanataaluma katika fursa za biashara.

“Tumejiandaaje kutumia taaluma hizo kwa uchumi wa viwanda, mchango wa wanataaluma katika kutambua fursa hasa kwa nchi zinazoendelea ni fursa zipi wanaziona na kuzifanyiakazi, wanazitambua na kuzitumia fursa hizo,” alisema Profesa Nyamsogoro.

Mkuu wa Shule ya Biashara chuoni hapo, Dk. Hawa Tundui, alisema hilo ni kongamano la tatu la kimataifa linalowashirikisha wanataaluma.

“Hili ni kongamano la tatu, la kwanza lilifanyika mwaka 2016 Zanzibar, la pili mwaka jana jijini Arusha na hili la leo, lengo ni kuwaunganisha wanataaluma wanaofanya tafiti zao na mchango wa wanataaluma kwa kuzingatia sera za nchi yetu. 

“Matokeo ya makongamano yaliyopita ni kuanzishwa kwa jukwaa la pamoja kati ya wanataaluma na watendaji wakuu wa makampuni mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi ili kuhakikisha tunajua mahitaji ya soko na sisi tufanye nini kuboresha elimu yetu,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Pages