Wasanii 100% wa Kitanzania kuzuru mikoa 15 ili kukuza
vipaji vya nyumbani.
Tiketi za VIP kutolewa bure kwa wateja watakaonunua Tigo VIP
Pack.
Dar es Salaam, Septemba
18, 2018-Tamasha la
kusisimua zaidi la muziki na utamaduni Afrika Mashariki na Kati, Tigo Fiesta
2018 – Vibe Lama Lote sasa lipo tayari kukonga mioyo na 100% mziki wa nyumbani
katika mikoa 15 ya nchi.
Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2018 ni Vibe Kama Lote, ikiashiria burudani maridhawa
na ladha ya kumbukumbu zisizofutika zinazoendana na msimu huu nchini kote.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Meneja
wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alibainisha kuwa, msimu wote wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote utashuhudia
burudani 100% kutoka kwa wasanii wa kitanzania, kufuatia mafanikio makubwa ya
mfumo uliotumika mwaka jana. Shangwe zinatarajiwa kuanza mjini Morogoro siku ya
Jumamosi tarehe 29 Septemba.
‘Muziki ni nguzo muhimu ya kampuni yetu, kwa hiyo Tigo
Fiesta 2018 itadumisha asili yake ya kuvumbua na kukuza vipaji vya Kitanzania.
Lengo letu kuu ni kukuza tasnia ya muziki na kutoa fursa za ajira kwa vijana na jamii yote kwa
ujumla’ William alisema.
Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote,
Gardner G. Habash alisema kuwa katika historia yake ya miaka 17, Tigo Fiesta imekuwa
jukwaa la kukuza muziki wa nyumbani. ‘Tigo Fiesta inawapa fursa wasanii
kuonesha uwezo wao na kuongeza idadi ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Kuna maelfu
ya mashabiki wanaohudhuria matamasha yenyewe au kufuatilia matukio kupitia
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,’ alisema.
Mbali na kutoa burudani ya uhakika, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote pia itaibua
fursa nyingi za kujiongezea kipato kwa wasanii pamoja na wakaazi wa maeneo mbali
mbali yatakayoshuhudia shamrashamra za msimu huu.
Pia
katika msimu huu wa burudani, Tigo inatoa tiketi za
watu mashuhuri (VIP) za kuhudhuria Tigo Fiesta 2018 kwa wateja ambao watanunua
vifurushi vya Tigo VIP Pack ambavyo vinawapa wateja huduma bora zaidi za
sauti, SMS na data kuanzia TSH 30,000/-. Vile vile, wateja wote wa Tigo pia
watapata nafasi ya kujishindia zawadi kem kem kama vile pesa taslim na simu
janja kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo ambapo
watatakiwa kujibu maswali yanayohusu Tigo
Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote.
‘Wasanii wenyewe pamoja na jamii yote kwa ujumla katika
mikoa 15 itakayotembelewa na msimu huu wa Tigo
Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote watapata fursa kubwa za kiuchumi zinazoendana
na msimu wenyewe,’ William alisema. Wafanya biashara mbali mbali ikiwemo
wamiliki wa hoteli, migawa, kumbi za starehe, mama niitilie, wauzaji wa nguo na
wamiliki wa vyombo vya usafiri huongeza kipato kutokana na biashara zao
kuchangamka kutokana na idadi kubwa ya wateja wanaohudhuria matamasha ya Tigo
Fiesta.
Gardner aliongeza kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote utajumuisha
miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara,
Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele
kikifanyika Dar es Salaam.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es salaam katika uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa
burudani za muziki katika mikoa 15 ya
nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mtendaji wa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) pamoja na Katibu
Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati).
No comments:
Post a Comment