Baadhi ya Wanasheria walio katika utumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria hao, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome mara baada ya kufunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
DODOMA, Tanzania
Wanasheria walio katika utumishi wa umma nchini, wameaswa kuhakikisha wanaandaa mikataba yenye manufaa kwa serikali hasa katika kipindi hiki ambapo serikali inahamasisha watu mbalimbali ndani na nje ya nchi kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mhe. Mkuchika amesema, Wanasheria wana jukumu kubwa la kuishauri serikali ili kuingia katika mikataba yenye manufaa kwa watanzania.
“Moja ya lawama mlizokuwa mkizibeba huko nyuma, ni kutoishauri serikali ipasavyo na kuingia katika mikataba mibovu ambayo inaleta matatizo wakati wa utekelezaji,” Mhe. Mkuchika amesema.
“Moja ya lawama mlizokuwa mkizibeba huko nyuma, ni kutoishauri serikali ipasavyo na kuingia katika mikataba mibovu ambayo inaleta matatizo wakati wa utekelezaji,” Mhe. Mkuchika amesema.
Mhe. Mkuchika amesisitiza kuwa, Wanasheria katika utumishi wa umma ni kada muhimu kwa kuwa wanasimamia tafsiri ya masuala mbalimbali ya mikataba, uendeshaji wa mashauri ya jinai na madai, uandishi wa sheria na kanuni zinazohusu utekelezaji wa sheria hizo, hivyo ni muhimu kada hii ikatimiza wajibu wake ipasavyo ili kuleta chachu kubwa mno ya maendeleo ya nchi.
Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Wanasheria wote katika utumishi wa umma ni vema wanapotekeleza majukumu yao wakajikita katika misingi ya maadili ya kiutumishi na kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu na wakati wote kujiepusha na mgongano wa masilahi na waajiri wao, kujiepusha na rushwa na vitendo ambayo ni kinyume na taratibu na maadili ya utumishi wa umma.
Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka Wanasheria hao kutoa ushirikiano kwa taasisi za utawala bora na kuhakikisha wanakataa rushwa na kuwafichua wala rushwa na wahujumu uchumi.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi ameahidi kuyazingatia maelekezo yote yaliyotolewa.
Mada zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na misingi ya taaluma ya tasnia ya sheria katika utumishi wa umma, masuala ya sheria ya uchumi na nafasi ya wanasheria katika utumishi wa umma kwenye uchumi wa viwanda, ujenzi wa mahusiano endelevu kitaasisi na mwelekeo wa tasnia ya sheria nchini.
IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINIOFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 1 Septemba, 2018
No comments:
Post a Comment