HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 16, 2018

BASI LA NEW FORCE LAPATA AJALI NA KUSABABISHA MAJERUHI

Mnamo tarehe 16/10/2018 majira ya saa 13:00 mlima Kitonga katika Barabara Kuu ya Iringa - Morogoro Wilaya ya Kilolo na Mkoa wa Iringa, Gari lenye namba za usajili T 852DHA aina ya ZHONGTONG BUS mali ya NEWFORCE wa Dsm likiendeshwa na IDD s/o BAKARI MALULI, kabila Mhehe, miaka 38 na mkazi wa Dsm akikwepa gari lenye namba za usajili T.623DMG, likiendeshwa na RAMADHAN S/O SALIMIN ambapo basi hilo la Kampuni ya New force kwa kuepuka kugongana uso kwa uso liliacha barabara na kupinduka hatimaye kusababisha majeruhi 12 ambao ni
1.LEONARD s/o POTES, KYUSA, 32 YRS WA MPANDA
2.JAMES s/o NDUNGURU, MNGONI, 49YRS, WA DSM,
3.IDD s/o BAKARI MALULI, MHEHE, 38YRS, DEREVA WA DSM
4.BAKARI s/o ZAYUMBA, MBONDEI, 27YRS WA MBEYA
5.NDEKE S/o MWAIFUSE 53YRS, WA DSM
6.TABIA d/ o FRANCIS, KYUSA, 65YRS, WA MBEYA
7 .GRACE D/o BONIPHACE, MCHAGA 24YRS, WA MOROGORO
8.GRORY D/o BONIPHACE MCHAGA 24YRS, WA MOROGORO
9.ANNA D/o ALEX 22YRS, MUHAYA, WA DSM
10.AZIZA D/o MUHINA, MZIGUA, 43YRS WA DSM
11.SAWA s/o MTINGALA MAKUA, 52YRS, WA DSM
12.IAN D/o EVANCE 2YRS, KYUSA WA MBEYA
waliolazwa hospitali teule ya Itunda wilaya ya Kilolo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari namba T623 kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari.

Amedhibitisha Kaimu RPC Kamishna Msaidizi wa Polisi. DEUSDEDIT KASINDO.

No comments:

Post a Comment

Pages