Mkuu wa Wliaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amekiri kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi kwenye Wilaya hiyo, ambapo amesema migogoro hiyo inaibuka kutokana na kutengenezwa na watu.
DC Chongolo ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo la Uchimbaji Kokoto katika eneo la Boko jijini Dar es Salaam, eneo lililokumbwa na migogoro baina ya Wawekezaji na Wachimbaji hao.
Akizunguma na Globu ya Jamii na Michuzi TV, Mhe. Chongolo amesitisha shughuli za uchimbaji kokoto katika eneo hilo mpaka watakapokaa kwa pamoja Novemba Mosi 2018, kati ya Wachimbaji wa Kokoto,wamiliki wa eneo na Serikali ili kusuluhisha mgogoro huo ikiwa sambamba na kuangalia namna ya kuendelea au kuacha shughuli hizo.
Chongolo amesema katika maeneo hayo ya uchimbaji watahakikisha yanakuwa na Leseni ya Manispaa, Leseni ya Madini, Cheti cha TRA, Mazingira, Mikataba kwa Waajiriwa, Malipo ya ushuru wa Madini kwa Manispaa na usajili katika uzalishaji Madini. "Kwenye haya maeneo ya uchimbaji Kokoto wanachimba kiholela, uharibufu ni mkubwa sana, magari yanapita juu chini wamechimba mashimo, mvua ikinyesha wanakimbilia wanajificha kwenye haya mashimo, ikileta madhara kwa watu malalamiko yote yanakuja kwa Serikali’’, amesema DC Chongolo.
Kwa upande wake mmoja wa Wawekezaji katika eneo la Boko, Mwakilishi wa Kampuni ya Usafirishaji na Uchimbaji wa Kokoto ya Al-Hushoom Evestment, Badi Lema amedai wao ni wamiliki halali wa eneo hilo, amesema kuna Watu wamevamia eneo hilo hivyo waliiomba Serikali ifike kwenye eneo hilo kujionea uvamizi huo.
Badi amesema licha ya kulinda eneo hilo, Wavamizi hao wameendelea kuingia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji wa kokoto. Hata hivyo moja ya Wananchi wanaofanya shughuli hizo za Uchimbaji amedai kuwa eneo hilo wamepewa na Wazo, wamedai eneo hilo walipewa kama Wananchi wa Boko. Pia baadhi ya Wachimbaji hao wamedai kuwa ruhusa ya Uchimbaji Kokoto katika eneo hilo la Boko wamepewa na Serikali ya Mtaa.
Baadhi ya Wachimbaji wa Kokoto wakiendelea na shughuli zao katika eneo linalodaiwa kuvamiwa na watu hao,ikiwemo uvunjwaji wa sheria za utunzaji mazingira,na utaraibu wa kuchimba kokoto hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akizungumza mbele ya Wachimbaji Kokoto katika eneo la Boko,ambalo linadaiwa kuvamiwa na wananchi huku wakiendeleza shughuli za uchimbaji bila kufuata utaratibu/sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akiwa na watalaamu wake wakiondoka kwenye eneo hilo la wachimbaji Kokoto eneo la Boko,mara baada ya kujionea hali halisi na kuamuru uchimbaji kokoto katika eneo hilo usitishwe mara moja,mpaka hapo watakapokutana siku ya Alhamisi na kuamua nini kifanyike.
Mmoja wa wachimbaji Kokoto katika eneo hilo akieleza jambo kwa mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo (hayupo pichani),aliyefika kujionea halisi ya eneo hilo.
No comments:
Post a Comment