*Ni baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanancho juu ya kutoridhishwa na fidia
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagizaMthamini
Mkuu wa Serikali Bibi. Evelyne Mugasha kwenda katika Kata ya Kiomoni
kufanya tathmini ya ardhi ya wananchi ili kubaini thamani halisi ya
maeneo hayo ili wananchi waweze kufidiwa.
Hatua
hiyo inakuja baada ya wananchi hao kumlalamikia Waziri Mkuu kuhusu
kutoridhishwa na fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na kampuni ya Neelkanthinayomiliki kiwanda hicho cha kuzalisha chokaa.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Oktoba 30, 2018) wakati
akizungumza na wananchi wa kata ya Kiomoni katika mtaa wa Kiomoni
wilayani Tanga akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya
siku tatu mkoani Tanga.
Alisema
atamtuma Mthamini Mkuu aende kubaini nani anadai nini na anamiliki nini
ili atoe kibali cha ulipwaji ili muwekezaji aweze kupewa kibali cha
kuwalipa fidia yao.”Tunataka jambo hili liishe kabla ya mwishoni mwa
mwaka huu kila kitu kiwe kimekamilika na hakuna mwananchi hata mmoja
atakayepoteza haki yake ya msingi.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa uwekezaji huo ni muhimu kwa kuwa ni sehemu ambayo
viwanda mbalimbali vya saruji nchini vinategemea kwa kupata malighafi,
hivyo alimpongeza muwekezaji na kumshauri aongeze uzalishaji kadiri
anavyoweza.
Alisema
wawekezaji katika sekta ya viwanda ni muhimu kwa sababu wanaunga mkono
mkakati wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli ya kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa
kupitia sekta ya viwanda.
Alisema
fursa ya uwepo wa kiwanda hicho utawezesha kukuza uchumi Taifa na
wananchi kwa ujumla kwa sababu kiwanda kitakapokamilika kitatoa ajira ya
watu zaidi ya 2,000 wakiwemo wakazi wa eneo hilo.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Bw. Thobias Mwilapwa
Mkinga leo (Jumatano, Oktoba 31, 2018) akutane na wananchi wa kijiji
hiko na kusikiza kero mbalimbali zinazowakabili na kushirikiana nao
katika kuzipatia ufumbuzi.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia
wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi
anawajibika kwa kiwango kinachostahili, ambapo aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kwenda kwa wananchi.
“Watendaji
hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekana
wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa
jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za
ngazi ya halmashauri,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, OKTOBA 31, 2018.
No comments:
Post a Comment