HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 16, 2018

HALOTEL YAADHIMISHA MIAKA MITATU YA KUTOA HUDUMA TANZANIA

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Halotel wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo kutoa huduma za mawasiliano Tanzania tangu ilipozinduliwa  nchini mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Son, na  kushoto ni Katibu wa  Kampuni hiyo, Nguyen Thi Thuy Linh.


Dar es Salaam, Tanzania
HALOTEL inakusudia kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani  Milioni 700 katika sekta ya mawasiliano nchini ikiwa na malengo ya kuwa nafasi ya pili na kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza.

Pamoja na mipango hiyo hiyo, tumekusudia kuendelea kuiboresha huduma yetu ya utumaji wa pesa kwa njia ya Mtandao ijulikanayo kama ‘Halopesa’ sambamba na kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ‘ICT’ kwa ajili ya wateja wa Mashirika Binafsi na Serikali kwa ujumla.

Katika kipindi hiki cha miaka mitatu tunapoadhimisha siku hii, Halotel tayari imefanya uwekezaji unaofikia Dola za Marekani Milioni 500, ikiwa ndiyo kampuni inayoongoza kwa kuwekeza  miundombinu ya Mawasiliano sehemu mbalimbali nchini inayowafikia asilimia 95 ya wananchi wote ikiwa na vituo 4,400 vya  kupokea mawasioliano (BTS’s) kwa umbali wa Kilomita 18,300.

Mpango wa biashara wa Halotel zaidi umelenga kuwafikia watu walioko pembezoni mwa miji kwa kuwapa gharama nafuu za mawasiliano  huku ikiwa tayari imewafikia wananchi zaidi ya Milioni tatu sambamba na Milioni moja wengine waliojiunga na mtandao wa Halopesa
Hivi karibuni pia Halotel itawekeza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha huduma za mtandao na zaidi kuhakikisha inahimarisha mtandao wa 4G kwa wateja wake kote nchini.

Tutaendelea kuboresha huduma zetu mbalimbali tukiwa na lengo la kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 pamoja na watumiaji Milioni 3 wa huduma ya Halopesa baada ya miaka mitano kuanzia rasmi mwaka ujao , pamoja na kuboresha huduma kwa wateja wetu wakubwa kutoka Taasisi mbalimbali za kibiashara za Binafsi na Serikali.

Tunaamini kuwa kupitia huduma hizi tutakuwa tumeisaidia Serikali na taasisi zote za kibiashara kuendeleza utoaji wa huduma zao kwa ufanisi  wakati huu ambao pia tunatarajia kuandaa mfumo maalumu  kwa wateja wetu utakaowawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Kupitia mikakati mbalimbali ya Kampuni yetu, Tunaamini tutaweza kufikia lengho la kuwa kampuni namba mbili inayotoa Mawasiliano yenye tija hapa nchini.
Mbali na hiyo Halotel imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii inayoliwezesha Taifa kufikia malengo yake mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages