Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na
Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akizungumza jambo wakati wa kukabidhi
vifaa vya zima moto pamoja na hati ya shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) na
wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Utafiti) Idara hiyo Bw.Bashiru Taratibu walipotembelea Oktoba 15,
2018.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na
Uokoaji - SUKOS, Suleiman Kova akimkabidhi vifaa vya zima moto Mkurugenzi wa
Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said kwa ajili ya
kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto katika maeneo ya kazi.
Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Utafiti Idara
ya Uratibu wa Maafa Bw.Bashiru Taratibu akiangalia vifaa vya zima moto
vilivyokabidhiwa na Taasisi ya Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji –SUKOS Oktoba
15, 2018 kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akipokea maelezo
kutoka kwa
Meneja wa Oparesheni Bi.Rahma Kova wakati wa kukabidhi cheti cha
Shukrani ya ushirikiano uliopo kati ya SUKOS na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na
Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akikabidhi Hati ya Shukrani kwa
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe
walipomtembelea kukabidhi vifaa vya zima moto Ofisini kwake Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akiwa katika picha
ya
pamoja na Uongozi wa SUKOS Foundation walipotembelea Idara hiyo ili
kukabidhi
Vifaa vya Zima Moto pamoja na hati ya shukrani kwa namna Taasisi yake
inavyoshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo, Suleiman Kova.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment