Kiongozi wa Jopo la Msafara wa Wataalamu wa Kampuni ya Emerson, William Fernandes, akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya Mafuta na Gesi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petrogas Field Services, Greyson Kiondo, akitoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya Mafuta na Gesi nchini.
KAMPUNI ya EMERSON inayoongoza duniani kutengengeneza mitambo na vipuri zikiwemo mita za kupima kiwango cha Nishati ya Mafuta, vimiminika na gesi imetoa mafunzo bure ya siku moja kwa wadau wa tasnia hiyo nchini.
kizalendo ya Petrogas Field Services Ltd ambao ni wawakilishi wa Emerson nchini Tanzania kwa muda mrefu.
Akizungumzia kuhusu faida za mafunzo hayo katika kuelekea uchumi wa Tanzania ya Viwanda, William Fernandes ambaye ni kiongozi wa jopo la msafara wa wataalamu hao wa Emerson kutoka nchini Marekani alisema ni pamoja na kuwaelemisha wadau juu ya mambo makubwa ya kuzingatia katika ununuzi na ufungaji wa mita za mafuta na gesi.
Alisema kuwa kutokana na umaarufu iliyojijengea kampuni hiyo ya Emerson itatoa elimu kuhusu mitambo mbalimbali waliyotengeza ikiwemo mita za kupima kiwango cha vimiminika, gesi za aina zote ikiwemo na mafuta wakati wa kuhamisha umiliki kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi.
“Mita hizo zinaitwa ‘Micro Motion Coriolis Flow meters zenye umbo la herufl ‘U’ na Daniel Ultra Sonic Flow meters ambazo tayari zimefungwa na kuleta mafanikio makubwa kwenye mitambo mbalimbali nchini katika Kampuni za gesi na mafuta za TPDC, Pan African Energy na Maurel & Prom." alisema Fernandes.
Akizungumzia faida nyingine, Fernandes alisema ni kuwaelemisha wadau juu ya mambo makubwa ya kuzingatia wakati wa ufungaji wa mitambo ya gesi, vimimini na mafuta kwa ajili ya biashara.
“Mambo hayo muhimu ni kama vile umuhimu wa kuzingatia kigezo cha umbo 1a “U” na usahihi katika ununuzi wa flow meters ili kutokutoa mwanya wa kuibiwa ama kupunjwa katika uhamishaji wa umiliki wa mafuta na gesi."
Emerson ilianzishwa mwaka 1870 nchini Marekani na imekuwa ikitoa teknolojia na mitambo ya kuhamisha umiliki (custody transfer/mass flow metering) na kupima kiwango cha mpitisho (flow measurement) wa vimiminika vya aina zote ikiwemo mafuta na gesi kwa miaka 85 sasa.
No comments:
Post a Comment