Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua tangi la maji wakati
alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Luyehe katika kijiji cha
Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3,
2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu ubora wake wakati alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wafuatilie utendaji kazi wa watumishi kwenye maeneo kubaini kama wanakwenda kwa wananchi na kuwahudumia ipasavyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu ubora wake wakati alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wafuatilie utendaji kazi wa watumishi kwenye maeneo kubaini kama wanakwenda kwa wananchi na kuwahudumia ipasavyo.
‘Serikali
inahitaji kuona watumishi wa umma wanakwenda kwa wananchi kusikiliza
kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kushirikiana nao katika
kuzipatia ufumbuzi’’.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana (Alhamisi, Januari 3, 2019) wakati
akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji
cha Lugagala, wilayani Songea akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani
Ruvuma.
“Rais
wetu Dkt John Magufuli ni muumini wa maadili na mchapakazi ,ndio maana
amesisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kwenda kuwahudumia wananchi
katika maeneo yao, kwani baadhi yao hawana uwezo wa kufikia maeneo ya
kutolea huduma.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa ni vema kwa watumishi wa umma wahakikishe wanapanga
muda wa siku tatu kwa wiki kutoka maofini kwenda kuwahudumia wananchi
hususani waishio maeneo ya pembezoni.
Alitumia
fursa ya mkutano huo kuwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao
pamoja na watendaji wake waliopo kwenye maeneo mbalimbali nchini kwani
Serikali inatambua matatizo yao na kuahidi kuwa yatapatiwa ufumbuzi kwa
wakati.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa Serikali haina msamaha na watumishi wazembe, hivyo
wananchi waendelee kuwa watulivu na imani kwani watahudumiwa na ahadi
zote zilizotolewa na Rais Dkt Magufuli katika maeneo yao zitatekelezwa.
Kadhalika,
Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea asimamie zoezi la
kuwaondoa wananchi wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu
ikiwemo kilimo katika maeneo ya vyanzo vya maji kwa sababu watasababisha
vyanzo hivyo vikauke.
Awali,
Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Luyehela
kwenye kijiji cha Muungano Zomba, kuzindua kituo cha kuchotea maji cha
kijiji cha Lugagala na kukagua mradi wa ujenzi ya zahanati wa kijiji
hicho.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho na Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Naibu Waziriwa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa Serikali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 4, 2019.
No comments:
Post a Comment