March 24, 2019

BENKI YA NMB YAUNGANISHA ZAIDI YA TAASISI 300 KUPITIA MFUMO WA ULIPAJI NA UKUSANYAJI MAPATO YA SERIKALI GePG

Meneja Uendelezaji Biashara Benki ya NMB Makao Makuu, Masato Wasira, akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na Benki hiyo ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwenye Mkutano wa Wadau wa maji Nchini uliofanyika Jijini Dodoma. akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na Benki hiyo ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwenye Mkutano wa Wadau wa Maji nchini uliofanyika jijini Dodoma.

DODOMA, Tanzania

Benki ya NMB Nchini imeweza kuunganisha Taasisi zaidi  ya 300 Nchini pamoja na  Halmashauri 180 kwenye mfumo wa ulipaji na ukusanyaji wa mapato Serikalini (GePG).
Hayo yalielezwa na Meneja Uendelezaji Biashara wa Benki ya NMB, Masato Wasira, wakati alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa wadau wa maji Nchini uliofanyika Jijini Dodoma.
Wasira alisema kuwa Benki ya NMB nchini imeweza kuunganisha Taasisi mbalimbali  zaidi ya 300 zikiwemo halmashauri 180 kupitia mfumo wa ulipaji na ukusanyaji mapato ya Serikali (GePG).
Pia Wasira alisema  Mamlaka za maji 22 na Idara za maji 5 pamoja na bodi za mabonde ya maji 7zimeunganisha katika mfumo huo wa malipo kupitia Benki ya NMB.
Alisema kupitia mfumo wa GePG Wateja wanaweza kulipia miamala ya Ankara za maji kupitia mitandao ya simu za mkononi au matawi ya benki ya NMB 220  yaliyoaenea Nchini nzima.
Aliongeza kuwa wateja hao wanaweza kulipia Ankara zao maji kupitia mawakala wa benki ya Nmb zaidi ya 6000 ,Internet banking  na kupitia huduma ya NMB mobale.
Aidha alisema Benki hiyo inawateja zaidi ya milioni 2.5 na kuweza kutoa ajira kwa Wafanyakazi zaidi  ya 3000 na inapatikana karibu Wilaya zote Nchini.
Alisema inatoa huduma kwa makundi yote kuanzia kwa wafanyabiashara,Wakulima,Makampuni,Taasisi na Serikalini.
Kwa upande wake Meneja mwandamizi mahusiano Serikalini Benki ya Nmb Makao makuu , Amanda Feruzi alisema benki ya NMB ilipata faida ya zaidi ya bilioni 106 baada ya kodi.
Alisema kupitia ukusanyaji mapato ya Serikali imeweza kusaidia Serikiali kutimiza mipango yake kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Aliongeza kuwa benki hiyo imeweza kutoa huduma mbalimbali za kifedha zenye kutoa suluhisho za changamoto zetu zinazotukabili nchini.
Kupitia utoaji huduma bora unaotolewa na benki ya NMB Nchini ,benki hiyo imetajwa na Taasisi ya Kimataifa ya Euromoney kuwa benki bora Tanzania mara sita.

No comments:

Post a Comment

Pages