NA MWANDISHI WETU
HASSAN
Mwakinyo oyeeeee! Tanzania oyeeee! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya bondia huyo kumtwanga mpinzani wake, Sergio Gonzalez
raia wa Argentina kwa TKO.
Katika
pambano hilo la raundi nane lililopigwa jijini Nairobi, lilimshuhudia
Mwakinyo akiibuka mbabe raundi ya tano tu baada ya kurusha makonde
mfululizo ambayo yalimshinda mpinzani wake huyo.
Mchezo
ulianza taratibu katika raundi ya kwanza na ya pili, huku mabondia wote
wakionekana kusomana mbinu wakati kila mmoja wao akijilinda zaidi hali
iliyofanya mchezo kuwa wa pande zote mbili.
Hadi
raundi ya pili inamalizika, Mwakinyo alionekana kushindwa kupenyeza
makonde kwenye uso wa Gonzalez ambaye alionekana kujilinda vyema.
Zikiwa
zimesalia sekunde chache kumalizika kwa raundi ya tatu, Mwakinyo
alicharuka na kumrushia makonde mfululizo mpinzani wake hali iliyoufanya
umati wa mashabiki kwenye Ukumbi wa KICC kuripuka kwa hoi hoi, nderemo
na vifijo.
Gonzalez
alirudi kwa kasi ya ajabu katika raundi ya nne kwa kumshambulia Mwakinyo
mfululizo, huku akirusha mkonde kwa mkono wake wa kushoto ulioonekana
kuwa na nguvu muda wote wa mchezo.
Wakati
kila shabiki akiamini kuwa huenda pambano hilo lingeamuliwa kwa pointi,
Mwakinyo alirudi kwa kasi ya ajabu katika raundi ya tano na kurusha
makonde mfululizo ambayo yalimshinda Gonzalez.
Mwakinyo alionekana kutumia vyema udhaifu wa Gonzalez upande wake wa kushoto ambao alikuwa akiulinda muda mwingi wa mchezo.
Makonde
mawili ya nguvu kutoka kwa Mwakinyo yalitosha kumpeleka chini Gonzalez
ambaye alishindwa kunyanyuka hali iliyomfanya mwamuzi kuamuru kumalizika
kwa pambano hili.
Kufuatia
ushindi huo, maelfu ya mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi Kombezi jijini Tanga, uliripuka kwa hoi hoi, nderemo na vifijo.
Umati
huo wa wana Tanga ulikusanyika katika maeneo ya Makorora ambapo ndipo
Mwakinyo alipozaliwa ili kumuunga mkono kijana wao huyo ambaye ni balozi
wa kampuni ya SportPesa.
Kila
mmoja aliyefika uwanjani hapo alionekana kurekodi kilichokuwa kikijiri
kwenye runinga kubwa iliyotumika kurusha mchezo hiyo kwa kutumia simu
yake ya mkononi huku furaha ikitanda kila kona.
Hili
litakuwa ni pambano la 15 kwa Hassan Mwakinyo kuibuka na ushindi baada
ya kushuka ulingoni mara 17 katika mapambano ya kulipwa, huku akipoteza
mawili tu kati ya hayo tangu alipoanza kujihusisha rasmi na ngumi za
kulipwa mwaka 2015.
Mtanzania
mwingine, Iddi Mkwera, alimchapa Mkenya Nicholas Mwangi kwa TKO katika
pambano la utangulizi la kumsindikiza Fatuma Zarika na Catherine Phiri
wa Malawi la kuwania ubingwa wa dunia wa WBC kwa wanawake.
Bondia wa Argentina Sergio Gonzalez akiwa chini baada ya kupata kichapo kikali kutoka kwa bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo.
Bondia wa Argentina Sergio Gonzalez akiwa chini baada ya kupata kichapo kikali kutoka kwa bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo.
Mwamuzi akihesabu kabla ya kumaliza pambano.
Sergio Gonzalezakiwa hoi.
Mwamuzi akimaliza pambano hilo baada ya
Sergio Gonzalez kushindwa kuendelea katika raudi ya 5.
Sergio Gonzalez kushindwa kuendelea katika raudi ya 5.
Hassan Mwakinyo akiwa na wasaidizi wake.
Mwamuzi akimtangaza mshin di wa pambano hilo bondia Hassan Mwakinyo kutoka Tanzania.
Sergio Gonzalez akisaidia kutoka katika ulingo baada ya kuchapwa katika raaundi ya 5
Mwakinyo akipongezwa.
No comments:
Post a Comment