NA MWANDISHI WETU
TIMU ya Taifa ya walemavu wa akili, wanatarajia kuwasili
nchini leo Machi 22 ikiwa na medali 15 kutoka katika michezo ya Dunia ya walemavu wa
akili iliyomalizika Falme za Kiarabu (UAE).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT),
Charles Rays katika medali hizo, 12 za
dhahabu, fedha moja na Shaba 2 zilizopatikana katika Riadha na Mpira wa Wavu.
Rays alisema michezo hiyo iliyochezwa UEA, michezo ya Riadha
ilichezwa Abu Dhabi huku Mpira wa Wavu michezo hiyo ilifanyika Dubai.
Katika mpira wa Kikapu, Tanzania imeibuka mabingwa baada ya
kuiadhibu Italia kwa seti 2-1 katika fainali.
Rays alisema katika riadha Tanzania imezoa medali 9 za
dhahabu , Fedha moja na shaba 2 ambako Boniventura Anga wa Mtwara alipata
medali ya dhahabu.
Aidha katika michezo hiyo, Tanzania ilishiriki michezo hiyo
sambamba na wachezaji kutoka kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nyarugusu.
Katika mapokezi hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge anatarajia kuwapokea wanamichezo hao ambao
wameiletea heshima Tanzania katika michezo hiyo.
Michezo ya dunia ya majira ya kiangazi yalianza Machi 14 na
kumalizika Machi 21 (UAE).
No comments:
Post a Comment