Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni
akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu alipotembelea Shamba
la Miti la Biharamulo mara baada ya
kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani
Geita. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).
GEITA, Tanzania
GEITA, Tanzania
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa
miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu
ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao
bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu.
Ametoa
muda huo ili wananchi waliolima mazao mbalimbali yakiwemo mahindi
na pamba waweze kuvuna mazao yao kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum
ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu
itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa
kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.
Mhe.Kanyasu
ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea shamba
la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Amesema
Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea
kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366
vilivyokutwa ndani ya Hifadhi.
Amesema
haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa
kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na
vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.
Amebainisha
kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na
kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata
wale waliokuwa wakiishi katika maeneo mengine nje ya hifadhi
waliendelea kuvamia na kuanza kujimilikishia maeneo makubwa wakidai
kuhalalishwa na tamko la Rais.
Amefafanua
kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi na timu ya Mawaziri na
Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya
vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali.
Kufuatia
hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo
mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi
linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa
kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa
miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu
Katika
hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa
wavamizi ndani ya Shamba hilo.
Ameitaka
TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue
Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote.
Awali,
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo
alisema kuwa baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua
wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo,
suala ambalo ni kinyume cha sheria.
Mkuu
huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana
mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia
hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.
Kwa
upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima amemweleza Naibu
Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya
Shamba hilo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na
vitendea kazi.
No comments:
Post a Comment