HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 27, 2019

Yanga yapigwa faini tena

NA JOHN MARWA
KLABU ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni sita (6,000,000) kwa makosa mawili waliyoyafaanya wakati wa mechi yao na KMC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wamekutwa na kosa la kupita mlango tofauti kuingia uwanjani faini yake milioni 3,000,000.


Kosa  la pili wakati wa mapumziko katika mpamabano huo hawakuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, faini milioni 3,000,000.


Jumla ya faini ni Kiasi cha shilingi za kitanzania milioni sita kutozwa Yanga ikiwa ni mara ya tatu mtawalia wanarudia makodsa hayo msimu huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi TPLB , Steven Mnguto, amesema kujirudia kwa makosa hayo kunatokana na udhaifu wa kanuni huku akibainisha kuwa msimu ujao watakuja na kanuni kali kudhibiti matukio hayo amabayo yanaonekana kuota mizizi.

No comments:

Post a Comment

Pages