Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo Mei 20, 2019 wakati wa kusaini mkataba
wa ushirikiano wa kibishara na Kampuni ya Visa Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Olive Njoroge. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Olive Njoroge, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mkataba
wa ushirikiano wa kibishara na Halotel. Kulia ni Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung.
Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo Mei 20, 2019 wakati wa kusaini mkataba
wa ushirikiano wa kibishara na Kampuni ya Visa Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Olive Njoroge na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Halopesa, Magesa Wandwi.
Baadhi ya waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Halopesa, Magesa Wandwi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa kibiashara na Visa Tanzania.
Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung, akisaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Olive Njoroge.
Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Olive Njoroge (kushoto), akibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung.
Kuchukua taswira.
NA MWANDISHI WETU
IDADI ya watumiaji wa Halopesa imeongezeka kwa
asilimia 71. 76 katika kipindi cha mwaka 2018, ikiwa ni kipindi cha mwaka mmoja
wa huduma zake.
Kampuni hiyo iliyofunguliwa mwaka 2017, wakati huo
ikianza na watumiaji wa Halopesa wapatao 780, 000, kwa sasa inajivunia
mafanikio.
Hii ni kutokana na idadi hiyo sasa kufikia jumla ya
watumiaji milioni 1.3, hadi mwishoni mwa mwaka 2018.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa
jana, Halotel Tanzania na Visa zimesaini mkataba wa kimkakati ambao
utawawezesha watumiaji wa Halopesa kufanya malipo kwa njia ya Visa kupitia simu
zao.
Kwamba, ushirikiano wao utawezesha watumiaji wa
Halopesa kutumia huduma ya Visa kwenye simu zao kwa kufanya malipo ya bidhaa na
kuweka pesa na kutoa kwa mawakala wa huduma ya Visa.
Takwimu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) iliyotoa mwaka 2018 inasema kuwa Halopesa ni huduma ya malipo kwa njia
ya simu inayokua kwa kasi sana hapa Tanzania.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, hata idadi ya wateja
waliojisajili kwa huduma ya Halopesa imeongezeka kwa kiasi cha asilimia 71.76
katika kipindi cha mwaka 2018.
“Kwa ukuaji mkubwa wa idadi ya wateja wa Halotel na
kuwa ni mtandao wa simu unaokua kwa haraka hapa Tanzania tangu tuanze kutoa
huduma hapa nchini, tunaamini idadi ya watumiaji wa Halopesa pia itaendelea
kuongezeka,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung.
Dung amesema
kuwa kwa sasa Halopesa ina zaidi ya mawakala 40.000 na kwamba nguvu ya mduma ya
Visa mama Ha‘opesa mama“: na uwezo zaidi wa kuwezesha wateja kufanya manunuzi
kwa “313 ya Visa kupitia simu zao.
“Kupitia ushirikiano huu, Halopesa itawapa wateja
kulipa kwa muuzaji kwa kutumia msimbo (code) iliyoko kwenye huduma ya Visa
kwenye simu zao.
Alisema, huduma hii ya Visa katika simu huwezesha
wateja kupata fedha zao moia kwa moja kutoka katika akaunti zao za benki
kupitia simu 230.
Hii ni pamoja na kulipia bidhaa kwa wauzaii, kutuma pesa bila gharama yoyote, kuweka pesa au kutoa pesa kupitia wakala yeyote wa huduma ya Visa,” alisisitiza Son.
Naye Mkurugenzi wa Visa nchini, Olive Njoroge,
ameelezea ushirikiano huo unalenga zaidi katika kuunganisha Watanzania kwenye
huduma ya Visa na kuleta usalama wa fedha zao kufanya malipo fanisi kwa huduma
na bidhaa.
‘Tunafarijika kwa ushirikiano huu kati yetu na
kampuni muhimu ya huduma za mawasiliano ya simu kama Halotel. Ushirikiano wetu
na Halotel utawafanya Watanzania kulipa kwa kutumia Visa katika simu zao
kupitia zaidi ya wachuuzi wapya 40,000.
Aliongeza kuwa, itawasaidia kupanuka kwa wigo wa
Watanzania wanaotumia huduma za kifedha hapa nchini.
Kupitia huduma ya Visa, muuzaji atapewa msimbo (QR
code) pamoja na namba maalum ya wakala
ambayo mteja ambaye simu yake ina huduma ya Visa
ataitumia kwa ajili ya malipo kupitia simu yake.
Alisema ushirikiano huu unadhihirisha nia Ya dhati
ya VISA kutanua wigo wa malipo kupitia Huduma za kifedha kwa njia ya simu
Ulimwenguni kote.
No comments:
Post a Comment