Wanafunzi wa kikundi cha Brass Band
kutoka Shule ya Msingi St. Home wakiongoza Maandamano ya Wanafunzi wenzao
katika kilele cha Mazimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika leo
katika Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Kwa kipindi cha Miezi
tisa Julai 2018 hadi Machi 2019 Jumla ya Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa
ikilinganishwa na mashauri 13382 ya mwaka 2017/18 hali ambayo ni sawa na
ongezeko la 34% ya migogoro ya ndoa hapa Nchini.
Akiongea kwa niaba ya
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
Mkurugenzi wa Watoto wa Wizara hiyo Bi. Mwajuma Magwiza aliitaja changamoto ya
maadili ya mmomonyoko wa maadili kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa hapa Nchini.
Bi. Magwiza aliongeza
kuwa Vitendo vya ukatili kwa watoto ndani ya familia vimekithiri huku wahausika wakubwa wa vitendo hivyo
wakiwa wanafamilia hili likijionesha
katika takwimu za Jeshi la polisi za mwaka 2017 zinaonesha kuwa Jumla ya
matukio ya ukatili kwa watoto 13457 yameripotiwa na Jeshi la polisi.
Alivitaja vitendo
hivyo kuhusisha ukatili wa kingono wenye matukio 3,583, mimba za utotoni 1,323 akiongeza
kuwa taarifa jeshi hilo imeonesha matukio ya mikoa ya kipolisi yenye ukatili
mkubwa kuwa ni kinondoni matukio 2,426, Dodoma 1,283, Tanga 164, Tameke 984 na
Arusha Matukio 972.
Wakati huo huo Serikali
imewataka baadhi ya Wazazi Nchini kuacha
tabia ya kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike kama ilivyo kwa watoto
wa kiume jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali katika kuhakikisha usawa
wa kijinsia unatekelezwa katika nyanja zote bila ubaguzi wa kijinsia.
Akisoma hotuba kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhandisi
Happiness Mgalula ambaye pia ni Katibu Tawala Masaidizi Mkoa wa Dodoma
aliongeza kuwa ni lazima elimu itolewe kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Aidha Bi.
Mgalula amewataka wazazi na walezi
kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wote bila kujali jinsia ikiwa ni hatua
muhimu ya kutekeleza ahadi ya Rais kwa
vitendo ya utoaji elimu bure kwa wanafunzi hapa Nchini.
Bi. Mgalula aliongeza
kuwa Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la mila potofu akizitaja mila hizo
kuwa ni kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, haki ya wanawake kumiliki ardhi,
vipigo kwa wanawake akiutaja mkoa wa Dodoma kuwa wa pili kitaifa katika vitendo
vya ukatili hapa Nchini.
Aidha Bi Mugarula
amewataka wanafamilia kuhakikisha wanakuwa ana Afya bora kwa kuhakikisha
wanakuwa na vitambulisho vya Bima ya Afya, Elimu na akina mama wajawazito
kuhakikisha wanaenda hospitali ili kupata huduma ya Afya kwa mama na mtoto.
Kwa upande wake Afisa
Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Happy Hiza amesema Mkoa wa Dodoma umefanikiwa
kutoa elimu juu ya Makosa ya Jinai kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya jamii na
katika ngazi ya Jamii ili kuwezesha elimu ya malezi na makuzi kwa watoto katika
jamii.
No comments:
Post a Comment