Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb).
Na
Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali ya Tanzania inafanya
mazungumzo na Serikali ya Cyprus ili kuweza kutatua changamoto za malipo kwa
wateja walioweka amana zao katika Benki ya FBME ambayo ilifutiwa leseni ya
kufanya shughuli za kibenki hapa nchini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Hayo yameelezwa Bungeni
jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti maalaum Mhe. Asha Abdullah Juma, alieuliza kuhusu
hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwasaidia wananchi walioweka amana zao
katika Benki ya FBME.
Dkt. Kijaji alisema kuwa
zoezi la kukusanya mali na fedha zilizokuwa za Benki ya FBME katika taasisi
mbalimbali za fedha hasa zilizopo nje ya nchi, limekumbwa na changamoto za
kisheria kati ya Tanzania na Cyprus ambako benki ya FBME ilikuwa ikiendesha
sehemu kubwa ya biashara zake hivyo kusababisha ucheleweshaji wa ukusanyaji na
ugawaji wa fedha na ufilisi.
“Hakuna tarehe rasmi ya
kuanza kulipa fedha kwa sasa kutokana na uwepo wa kesi zinazokwamisha zoezi la
ukusanyaji mali na madeni ya Benki ya FBME”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa, Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 inaeleza kuwa amana au akiba za
wateja katika Benki au Taasisi zina kinga ya Bima ya Amana ya kiasi kisichozidi
Sh. milioni 1.5, na iwapo mteja ana
salio la amana la kiasi kisichozidi Sh. 1.5 atapata fidia ya asilimia 100.
Aidha wateja walio na
zaidi ya Sh. milioni 1.5 wanalipwa Sh. milioni 1.5 kama fidia ya bima ya amana
na kiasi kinachobakia kinalipwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Ufilisi.
Hata hivyo malipo kwa
mujibu wa Sheria na taratibu za ufilisi yanategemea makusanyo ya fedha kutoka
kwenye mauzo ya mali pamoja na fedha zilizowekwa na benki katika taasisi
mbalimbali za fedha za ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment