Meneja wa Huduma za Serikali wa NMB, Kanda ya Kati, Josephine Kulwa, akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na madawati wenye thamani ya Sh. Mil. 10 kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel. (Na Mpiga Picha Wetu).
SHULE ya Msingi Ukombozi na Sekondari Magungu, zilizoko Kiteto mkoani Manyara, zimepewa na kupokea msaada wa vifaa vya ujenzi na madawati kutoka Benki ya NMB, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 10.
Vifaa hivyo ni bati, misumari na mbao, vyenye thamani ya Sh. Mil. 5 kwa ajili ya Shule ya Msingi Ukombozi iliyopo Kata ya Engusero, na madawati yenye thamani ya Sh. Mil. 5 kwa Shule ya Sekondari Magungu, msaada uliokabidhiwa juzi.
Meneja wa Huduma za Serikali wa NMB Kanda ya Kati, Josephine Kulwa, akikabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel, katika vijiji vya Magungu na Engusero, alisema vifaa hivyo vinalenga kusapoti juhudi za Serikali kusimamia sekta kelimu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Josephine alisema: “Serikali inafanya mambo makubwa, sisi kama wadau tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuisaidia jamii kupata huduma kwa kiwango kinachotakiwa.”
Akipokea msaada huo, Mollel, alisema Sekta ya Elimu bado inakabiliwa na changamoto lukuki zikiwepo uhaba wa vyumba vya madarasa, Ofisi na nyumba za Walimu na madawati, ambazo zimekuwa kiini cha kufifisha maendeleo ya elimu na wanafunzi nchini.
NA
MWANDISHI WETU

“Bado kuna baadhi ya maeneo hapa Kiteto, watoto wetu wanasomea chini ya miti kwa kukosa vyumba vya madarasa pamoja na kwamba kuna jitihada kubwa za Serikali na taasisi zingine zisizokuwa za Kiserikali katika kusaidia sekta hii,” alisema Mollel.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamim Kambona, alisema kwa kipindi cha miaka minne, Serikali imeongeza vyumba vya madarasa na kupunguza adha kwa wanafunzi kusoma kwa kupokelezana madarasa na kuomba wadau wengine wa elimu kuendelea kusaidia kupunguza adha hiyo.
Kambona ametoa wito kwa jamii wilayani Kiteto, kutunza misaada wanayopata kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na hata Serikali ili iweze kutumika na kuleta tija kwa wananchi hasa katika kipindi hiki.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magungu, aliyejulikana kwa majina ya Bosiwa Mbali, alipongeza NMB Tawi la Kibaya kwa msaada huo, akisema wasingeweza kupunguza adha kwa wanafunzi kukaa chini mwaka huu kutokana na kutopata mazao kwa uchache wa mvua.
“NMB wametusaidia sana tusingeweza kununua madawati mwaka huu, hili liko wazi, hali yetu wazazi ni mbaya kiuchumi hivyo tatizo hili bado halijaisha tunaomba wadau wengine wajitokeze ili watusaidie kuondoa tatizo hili,” alisema Bosiwa.
No comments:
Post a Comment