NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wa Halmashauri
ya Wilaya ya Tabora (Uyui) wameazimia kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti na
pamba kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuvutia wawekezaji katika sekta ya
viwanda.
Azimio hilo limefikiwa na Wakulima 200 na viongozi 20 wa vijiji vya Miyenze na Lutende wilayani Uyui
baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali
na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA).
Akisoma maazimioa ya
wakulima Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema wakulima
wamekubaliana kulima ekari sita(6) za alizeti na ekari tatu za pamba na mazao
ya chakula kwa ajili ya kuinua uchumia wao.
Alisema ongezeko hilo la
kilimo linakwenda sanjari na mtumizi ya mbegu za kisasa za alizeti na kulima
kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuwa na malighafi nyingi
zitakazovutia wawekezaji kwenda Uyui.
Aidha wakulima hao pia
walikubaliana kuanza kuwa na kilimo biashara kwa ajili ya kuongeza tija katika
kilimo chao na kuondokana na umaskini unatokana na uzalishaji wa mazoea wa
uzalishaji wa kujikimu na kuelekea katika uzalishaji wa ziada.
Katika hatua nyingine
wamekubaliana kuanzisha chama cha Ushirika wa Wafugaji ili wawezeze kuunganisha
nguvu pamoja katika kutafuta huduma mbalimbali ikiwemo ya kupata dawa za mifugo
kwa urahisi na uuzaji wa bidhaa za mifugo kwa bei nzuri.
No comments:
Post a Comment