HABARI MSETO (HEADER)


May 14, 2019

WANATAALUMA WAPEWA MAFUNZO YA SIKU TANO YA KUWAJENGEA UWEZO KATIKA KUSIMAMIA MASOMO UZAMILI NA UZAMIVU

Wanataaluma kutoka katika Ndaki, Taasisi na Shule Kuu za Chuo Kikuu Dar es Salaam wameanza Mafunzo ya kuwajengea uwezo katika usimamizi masomo ya Uzamili na Uzamivu yanayotolewa chuo Kikuu Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 13 hadi 17 Mei 2019 katika Ukumbi wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii (CCE) cha Chuo Kikuu cha dar es Salaam.

Lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi katika usimamizi wa masomo pamoja na kuwasaidia wanataaluma hao kuwa na uwezo wa juu wa kusimamia kazi za wanafunzi katika taasisi nyingine za elimu ya juu.

Matarajio ya Mafunzo kwa wanataaluma hao ni kuwawezesha kuwa wakufunzi bora watakao waongoza wanafunzi wao katika kuandaa tafiti zao pamoja kuwapa mbinu bora za kuandaa tafiti zao.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Arnold Towo akizungumza na wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku Tano ya kuwaongezea ujuzi wa masomo ya Uzamili na Uzamivu yaliyoanza leo Tarehe 13 hadi 17 Mei,2019 yanayofanyika Chuo Kikuu Dar es Salaam.


Wanataaluma kutoka Ndaki, Taasisi na Shule kuu za Chuo Kikuu Dar es Salaam wakifuatilia maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma Dkt. Towo hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kusimamia masomo ya Uzamili na Uzamivu yanayofanyika kwa siku tano Chuo Kikuu Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 17 Mei,2019.

Prof. A. Ishumi kutoka Shule Kuu ya Elimu akiwaeleza wanataaluma kutoka Ndaki, Taasisi na Shule kuu za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lengo na madhuni ya Mafunzo hayo yaliyoanza ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Uzamili na Uzamivu yanayofanyika Chuoni hapo kwa siku tano kuanzia tarehe 13 hadi 17 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam.

Wanataaluma kutoka Ndaki, Taasisi na Shule Kuu za Chuo Kikuu Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Prof. A Ishumi alipokuwa akiwapitisha katika vipengele vya mafunzo watakayopatiwa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo kuanza leo tarehe 13 Mei, 2019 katika Ukumbi wa (CCE) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  hadi 17 Mei 2019 katika Ukumbi wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii (CCE) cha Chuo Kikuu cha dar es Salaam.

Lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi katika usimamizi wa masomo pamoja na kuwasaidia wanataaluma hao kuwa na uwezo wa juu wa kusimamia kazi za wanafunzi katika taasisi nyingine za elimu ya juu.


Matarajio ya Mafunzo kwa wanataaluma hao ni kuwawezesha kuwa wakufunzi bora watakao waongoza wanafunzi wao katika kuandaa tafiti zao pamoja kuwapa mbinu bora za kuandaa tafiti zao.

No comments:

Post a Comment

Pages