Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za
wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja za Mapato na Matumizi ya shilingi
trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini
Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza kuhusu
makusanyo ya kodi kuongezeka, wakati wa kuhitimisha hoja za wabunge kuhusu
Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa
Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za
wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni
Jijini Dodoma.
aadhi
ya wabunge na Mawaziri wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya
kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya
Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa tano kushoto), akiwa na
watumishi wengine wa Wizara hiyo, wakifuatilia mijadala ya wabunge kuhusu
Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni
Jijini Dodoma, ambayo ilipitishwa kwa kishindo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) (kushoto), akizungumza
jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili
kushoto), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha
na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) (kulia),
akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James,
baada ya Bunge kupitisha bajeti ya sh. trilioni 11.94 ya Wizara ya Fedha na
Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa kwanza kulia), akiwa na Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis
Mwakapalila, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaabani na viongozi
mbalimbali wa Wizara wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara iliyosomwa
bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
(hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara
hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bw. Doto James baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo nje ya
ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya
Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. George Simbachawene, nje
ya ukumbi wa Bunge baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo Jiijni Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wanne kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili
kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya
Wizara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
No comments:
Post a Comment