*Asisitiza kwamba madai yote kumalizwa ndani ya mwaka huu wa fedha
Lindi, Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia
wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa kuwa Serikali italipa fedha
hizo ambazo ni zaidi ya bilioni 20 mwaka huu.
Amesema
wakulima ambao bado hawajalipwa au kumaliziwa malipo yao baada ya
Serikali kumaliza uhakiki majina yao yatapelekwa TADB kwa ajili ya
malipo.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo Juni 1, 2019 katika kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Lindi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa
CCM mkoa.
“Wakulima
wote wanaodai malipo yao ya korosho watalipwa katika mwaka huu wa fedha
kwa kuwa ni haki yao na kwamba Serikali haitodhulumu haki ya mkulima
yeyote.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesisitiza suala la uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali
ya kutolea huduma zikiwemo barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi
wakati wote.
Amesema
uboreshwaji wa mbiundombinu pamoja na huduma nyingine za jamii ni
jukumu la watendaji, hivyo wahakikishe wananchi wote wanahudumiwa bila
ya kubaguliwa.
“Kila
aliyepewa jukumu ahakikishe analitekeleza ipasavyo. Watendaji
hakikisheni mnawatumikia Watanzania wote vizuri, kusiwe na ubaguzi wa
kisiasa, kidini na kikabila.”
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema zoezi la malipo ya fedha za korosho zilizohakikiwa linaendele.
Amesema
hadi Mei 31 mwaka huu kilo 51,990,999.97 zenye thamani ya sh. bilioni
171,570,299,912 ambazo ni sawa na asilimia 87.6 zimeshalipwa kwa
wakulima husika.
Mkuu
huyo wa mkoa amesema kiasi cha bilioni 23,404,086,508 bado hazijalipwa
kwa wakulima wa korosho wa mkoa wa Lindi. Korosho hizo zilihakikiwa
kituo cha Mtwara.
Kikao
hicho kimehudhuriwa na wabunge wa mkoa wa Lindi, Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na Wakuu wa Idara.
No comments:
Post a Comment