June 08, 2019

DC MUHEZA AWATAKA WAZAZI NA WALIMU KUHAKIKISHA KILA MTOTO ANAKUWA NA MTI MMOJA NYUMBANI NA SHULENI

MKUU wa wWlaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo wilayani imefanyika katika Kijiji cha Kimbo Kata ya Potwe Tarafa ya Bwembwera.
Mkurugenzi wa Mazingira Wizara Maji Obadia Kibona akizungumza wakati wa maadhimisho.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akipanda miti kwenye maadhimisho hayo.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio hayo.


Na Mwandishi Wetu

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanaasha Tumbo amewataka wazazi na na walimu kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mti mmoja shule na nyumbani ikiwa ni kampeni endelevu ya uhifadhiwa wa mazingira

Amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utaweza kuendesha kampeni endelevu ya uhifadhi wa Mazingira na vyanzo vya maji jambo ambalo litasaidia uwepo wa miti ya kutosha kwenye maeneo yenye vyanzo hivyo

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo wilayani imefanyika katika Kijiji cha Kimbo kata ya Potwe Tarafa ya Bwembwera.

Katika maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji,Bonde la Maji la Mto Pangani,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira( Tanga Uwasa),Umoja wa Utaunzaji Mazingira na Vyanzo vya Maji mto Zigi(Uwamakizi)na viongozi wengine wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza.

Amesema kuwa katika kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri na rafiki kila mwanafunzi anatakiwa kupanda miti miwili mmoja nyumbani na mwingine shule.

" Natoa agizo kwa wazazi na walimu kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa amepanda mti mmoja nyumbani na mwingine shule ili tuweze kuyatunza mazingira na vyanzo vya maji" alisema.

Aidha alisema mbali na hilo pia kuwe na utaratibu wa kila siku watoto wajengewe utaratibu wa kuokota takataka za mufuko ya plastiki inayozagaa ovyo.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa m Jumuiya ya Watumia Maji zigi juu Philipo Mdoe alisema baadhi ya wavuvi waliopo kwenye vijiji sita vilivyopo kata mbalimbali wilayani humo wanadaiwa kuvua kwa kutumia sumu za mimea na viwandani kwa ajili ya kuua samaki.

Alisema kwamba hatua hiyo imeanza kuleta hofu kubwa kwa watumiaji wa maji ya Mto Zigi ambao hutumiwa na wakazi zaidi ya 600,000 waliopo wilayani humo na Jiji la Tanga.

Aidha alisema uchunguzi walioufanya katika vijiji hivyo wamebaini kuwa sumu inayomwagwa kwa ajili ya kuua samaki ni ile ya mimea inayojulikana kwa jina la Deles ileya viwandani aina ya DIP inayotumika kuogeshea wanyama.

Akielezea udhibiti wanaoufanya kudhibiti vitendo hivyo,Mjumbe wa Kamati ya Mazingira Zigi Juu Awadhi Shauri alisema wavuvi hao hufanya kazi hiyo nyakati za usiku kuanzia saa nane mpaka saa tisa hivyo wanaiomba serikali na mamlaka husika kutoa msaada wa kwa sababu kamati za mazingira zilizoundwa hazikidhi mahitaji.

No comments:

Post a Comment

Pages