June 08, 2019

NHIF TANGA WATUMIA MAONYESHO YA SABA YA KIMATAIFA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU CHF ILIYOBORESHWA

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii .Constantine Kanyasu kushoto akimsikiliza kwa umakini Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati alipotembelea alipokwenda kufunga  maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii .Constantine Kanyasu kulia akipima uzito kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima Afya mkoani Tanga (NHIF) mara baada ya kulitembelea.
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu juu ya CHF iliyoboreshwa mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam ambaye alitembelea banda lao Devutia Kulembeka.
 Mhudumu wa Afya kulia akiendelea na shughuli kwenye banda hilo.
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao.
  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakipima afya zao.

Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga umetumia maonyesho ya saba ya biashara ya kimataifa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na CHF iliyoboreshwa ili waweze kujiunga nayo na kuweza kunufaika.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo mkoani hapa Ally Mwakababu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema wameona washiriki kwenye maonyesho hayo ili pia kutoa elimu ya bima ya afya kwa watumishi, wananchi binafasi, wanafunzi na watoto ikiwa ni mkakati wao wa kufikia watu wengi zaidi

“Tunashukuru kwenye maonyesho haya tumepata fursa ya kutoa elimu ya CHF iliyoboreshwa na nia kubwa ni kwamba kila mwananchi awe na kinga ya matibabu wakati wote”Alisema

Meneja huyo alisema licha ya kutoa elimu hiyo lakini pia wanafanya zoezi la kupima afya za wananchi wanaotembelea banda lao ikiwemo kupima uzito lakini pia wanapima sukari na baadae kutoa ushauri wa wananchi wanaopita kwenye banda lao.

Alieleza ushauri huo ni kwamba baada ya kupimwa wanatakiwa kufanye nini hivyo wanaamini wananchi wakitumia banda hilo watapata huduma ya vipimo bure na kupata ushauri mzuri.

No comments:

Post a Comment

Pages