June 11, 2019

Mahakama yahamuru Wema Sepetu akamatwe

NA JANETH JOVIN
Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu (pichani) yuko matatani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa hati ya kumkamata  kwa kuruka dhamana.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Hati hiyo ya kumkamata Wema imetolewa leo Juni 11 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, amedai mshtakiwa alifika Mahakamani lakini kaumwa hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha Mahakama.

Akitoa uamuzi Hakimu Maira amesema Mahakama inatoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

No comments:

Post a Comment

Pages