Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda, akizungumza na Masheikh na Walimu
wa Madrasa wa Wilaya hiyo nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada
ya kuwafuturisha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Masheikh na
Walimu wa Madrasa kutoka katika Wilaya ya Kinondoni, wakisikiliza nasaha kutoka
kwa Sheikh wa Wilaya Hiyo, Mohamed Muhenga baada ya futari iliyoandaliwa na
Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda nyumbani kwake jijini Dar es
Salaam Juni 2, 2019.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda
wakitoa mkono wa Idd kwa Masheikh na Walimu wa Madrasa wa Wilaya hiyo, Nyumbani
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuwafuturisha.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda
wakitoa mkono wa Idd kwa maustadhati wa Wilaya hiyo, nyumbani kwake Mikocheni
jijini Dar es Salaam jana baada ya kufu wa wafuturisha.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda
wakitoa mkono wa Idd kwa Masheikh na Walimu wa Madrasa wa Wilaya hiyo, Nyumbani
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuwafuturisha.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda
wakitoa mkono wa Idd kwa Masheikh na Walimu wa Madrasa wa Wilaya hiyo, Nyumbani
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuwafuturisha.
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Juma Mwenda na Mkewe, Tausi Sangawe Mwenda
wakitoa mkono wa Idd kwa Masheikh na Walimu wa Madrasa wa Wilaya hiyo, Nyumbani
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuwafuturisha.
Dar es Salaam, Tanzania
Meya Mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni ameahidi kugharamia mafunzo kwa ajili ya walimu wa Madrassa zilizopo katika Wilaya
ya Kinondoni kwa ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi walimu hao ili
kuongeza tija katika kueneza dini hiyo.
Meya Mwenda
alitoa ahadi hiyo wakati wa futari
aliyoiandaa maalumu kwa ajili ya walimu hao, wakiwemo maustadhi na
Masheikh wa Misikiti mbalimbali iliyopo katika wilaya hiyo akiitikia ombi la
Sheikh wa Wilaya ya Kinondoni Mohammed Mhenga aliyemuomba kufadhili mafunzo
hayo.
Katika
futari hiyo aliyokuwa ameiandaa katika makazi
yake Mikocheni Jijini Dar es Salaam, Mwenda alisema mafunzo kwa walimu hao ni
jambo asiloweza kulipa ugumu kwa kuwa anatambua thamani yao na hasa katika uenezaji na uendelezaji wa
dini hiyo.
“ Natambua
kazi nzuri mnayoifanya katika kufundisha dini ya Uislam hasa kwa watoto wetu na jamii ya watu wengine,
nimelipokea suala hili na nipo tayari kushirikiana nanyi wakati wowote
mtakaponiambia kuwa mpo tayari” alisema Mwenda.
Aidha alisema
kitendo chake na kuwaalika walimu hao na kufuturu nao pamoja, kimelenga
kuwatambua na kuthamini mchango wao mkubwa wanaoutoa kuiendeleza Quran ambayo
ilishushwa ndani ya mwezi wa Ramadhan maalumu kwa ajili ya waumini wa dini ya
kiislam pamoja na waamini wengine.
“Niwapongeze
kwa kazi nzuri mnayoifanya kuindeleza dini hii, kwa hakika mnabeba thawabu
kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, naamini siku moja atawalipa kama siyo hapa
duniani basi akhera” alisema Meya huyo Mstaafu.
Awali Sheikh
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mohammed Mhenga mbali na kumpongeza Mwenda kwa
hatua yake ya kufuturu na walimu hao, aliwataka walimu hao kuzidisha elimu
wanayoitoa kwa vijana kwa lengo la
kuzidi kuieneza dini hiyo.
Aidha
alisema kumalizika kwa mwezi mtukufu kusiwafanya waislam kubadirika na kugeuka
kutenda matendo yenye kumchukiza Mungu na badala yake waendelee kusimama
kikamilifu na kumuabudu mwakati wote.
No comments:
Post a Comment