June 17, 2019

MTOTO WA MCHUNGAJI APELEKWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UVAMIZI

Na Janeth Jovin

MTOTO  wa marehemu Mchungaji wa dhehebu la Evangelist Assemblies of God (EAGT), John Mfuko, ajulikanaye kwa jina la Frida Mfuko, amefunguliwa kesi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke kwa kile kilichoelezwa kuwa amevamia eneo lililoko keko juu katika kiwanja Na. 154 Plot II (Temeke) ikidaiwa kuwa kiwanja hicho ni mali ya dhehebu hilo  la EAGT.

Kesi hiyo Na. 127 ya 2019 ipo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza Amina. Aidha, dhehebu la EAGTE, imeonekana kuwa ni mdai  namba moja katika kesi hiyo. 

Wadai  wengine ni Mchungaji Sara Samson (ambaye pia amesema kuwa ni mdhamini wa muda wa dhehebu la EAGT), Wilbroad Adebe na Enosi Ndembeta ambao ni wazee wakanisa lililoko katika eneo hilo linalogombaniwa, wote kwa ujumla wakidai kuwa mtoto wa marehemu Mzee Mfuko, amevamia eneo hilo.

Akizungumza na blog hii, frida Mfuko anasema kuwa baba yake ni mmoja wa waazilishi wa dhehebu la EAGT tangu 1993 baada ya kutokea kwa mgogoro mkubwa katika kanisa la Tanzania Assemblies of God  (TAG). 

Anasema marehemu Mchungaji   Mfuko amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa EAGT  hadi pale  kifo kilipomkuta tarehe Agosti Mosi mwaka jana.

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa familia amedai kuwa tarehe Mei 9, 2013 wajumbe watatu wa bodi ya wadhamini walikaa kikao na kuidhinisha pamoja na mambo mengine kuwa,  kiwanja na. 154 kilichopo katika Kitalu II, Keko Juu, Manispaa ya Temeke si mali ya EAGT bali ni mali ya Marehemu mchungaji Mfuko na hivyo wadhamini waliaamua kumilikisha kiwanja hicho.

"Baraza la wadhamini lilifanikiwa kuandaa nyaraka za kubadilisha hati ya kiwanja hicho na kumilikisha rasmi marehemu mchungaji John Henry Mfuko na hivyo hati ya kiwanja ikabadilishwa kutoka jina la The Registered Board of Trustees of EAGT, na kuwekwa jina la John Henry Mfuko kama miliki halali wa kiwanja hicho na shule iliyopo katika kiwanja hicho amabayo pia imesajiliwa kwa jina hilo  la mchungaji," anasema 

Aidha, watoto wa marehemu mchungaji  Mfuko wamelaani kitendo hicho cha kuwataka kuwafukuza na kuwanyanganya mali ya baba yao ikiwa viongozi wa EAGT wanajua fika kuwa kiwanja kile pamoja na majengo yaliyopo na shule ni mali ya marehemu baba yao .

Aidha, msemaji wafamilia ameiambia  blog hii kuwa, viongozi wa EAGT, wanafanya unyama huo kwa sababu marehemu mzee mfuko kabla ya kufariki dunia  alikuwa akihoji viongozi wakuu wa kanisa la EAGT kuhusu tuhuma za kuingiza magari nchini kwa kutumia jina la EAGT ikiwa magari hayo hayapo ndani ya umiliki wa dhehebu hilo ikiwa kuna ukwepaji wa kodi ya serikali.  

Baadhi ya washirika na wachungaji wa dhehebu la EAGT waliohojiwa  walisitikishwa na kidendo hicho huku wakisema kuwa marehemu Mzee mfuko alikuwa nguzo muhimu katika dhehebu la EAGT na hivyo kuwanyanyasa watoto wake ni kutafuta laana. 

Aidha wamesikitishwa na vurugu zinazoendelea ndani ya dhehebu la EAGT kwa muda mrefu sana ambapo wachungaji wanafukuzwa katika makanisa yao na serikali haijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo.

 Wakati yote hayo yakiendelea viongozi wa EAGT wamekumbwa na tuhuma nzito zikiwemo za kuingia mikataba isiyowazi ya kupangisha majengo ya Makao Makuu yaliyopo Dar es Salaam Katika kiwanja namba 1 Barabara ya nyerere.
Kwa mujibu wa mpangaji katika eneo hilo (Imalaseko Super Market )  kupitia barua yake ya tarehe 3/4/2018 (kumb. Na. IIL/GN/003/2018) ni kuwa; kampuni hyo ilipewa jukumu la kujenga majengo hayo na kisha kuyatumia hadi hapo itakapokuwa imejirejeshea gharama za ujenzi . 

Hivyo kufikia tarehe 1/8/2018 Kampuni ya Imalaseko Investment Limited  ilikuwa imekaa katika majengo hayo kwa kipindi cha miaka saba (7) na ilikuwa imeweza kujireshea kiasi cha sh. 422, 204,720/=  na hivyo kuwa bado indai kiasi cha sh. 2,416,204,720/.

Kwa mujibu wa Mchungaji John Mahene, ambaye ni Makamu Askofu Mkuu wa EAGT, anasema kuwa si kweli majengo ya EAGT  yalijengwa tu kwa  gharama za Imalaseko Investment Limited bali makanisa yote nchini yalichangishwa ilikufankisha ununuzi wa kiwanja na majengo hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages