June 17, 2019

Wananchi watakiwa kutumia bidhaa zenye ubora

Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Cables ambacho kinazalisha mabomba ya Kisasa ya kupitisha nyaya za Umeme, Taliq Mohammed akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mabomba wanayozalisha.

Na Janeth Jovin

BAADHI ya wafanyabiashara ambao ni wazalishaji wa bomba za kupitishia nyaya za umeme wamesema kuwa wanashindwa kuendelea na uzalishaji kwa sasa kutokana na kuwepo kwa bidhaa feki masokoni. 

Wazalishaji hao wamedai kuwa kwa sasa kuna wingi wa mabomba feki katika masoko hivyo wanawaomba watanzania kuacha kununua na kutumia bidhaa hizo zisizokuwa na ubora  kwani uleta madhara makubwa majumbani mwao.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Cables ambao ni wazalishaji wa mabomba, Taliq Mohammed alisema wanaomba serikali iweze kutatua tatizo hilo kwa lengo la kuwaokoa wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo. 

Alisema kiwanda chao kimekuwa kikizalisha bidhaa ya mabomba ya kupitisha nyaya za umeme yenye ubora lakini wamekuwa hawafanyi vizuri sokoni kutokana na wingi wa mabomba feki yanayotoka nje ya nchi. 

"Kutokana na uwepo wa bidhaa feki masoko umesababisha mpaka sasa sisi wazalishaji wa ndani tunashindwa kuendelea na uzalishaji tunaiomba sana Serikali yetu iweze kutusaidia katika hili ili nasi tusifunge kiwanda hichi kwani mamia ya watanzania watapoteza ajira, " alisema.

Naye Ofisa Masoko wa Kiwanda hicho, David Tarimo, alisema ni muhimu kwa watanzania kununua bidhaa zenye ubora kwa lengo la kukuza uchumi na wao kuepuka kupata madhara mbalimbali. 

Alisema wao ni wazalishaji wa mabomba imara yenye ubora  ya kupitishia nyaya za umeme lakini wanashindwa kufanya vizuri sokoni kutokana  na uwepo wa mabomba feki. 

"Tunaiomba mamlaka husika idhibiti jambo hili kwa lengo la kiwasaidia wawekezaji wa ndani,  lakini Pia tunaendelea kuwasisitizia wananchi kutumia vitu venye ubora, " alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages