June 10, 2019

OFISA WA TRA, POLISI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA RUSHWA

 Watuhumiwa wa kosa la kuomba rushwa ya shilingi milioni mbili ambao ni askari Polisi wakitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019 kwa kosa la kushawishi rushwa ya shilingi milioni mbili kutoka mfanyabiashara wa Kariakoo.
Ofisa Msaidizi wa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charity Ngalawa (28), akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo baada ya kusomewa shtaka la kushawishi rushwa ya shilingi milioni mbili kutoka kwa mfanyabiashara wa Karikaoo, Ramadhani Ntunzwe.



Na Janeth Jovin

OFISA Msaidizi wa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charity Ngalawa (28) na askari Polisi wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka moja la  kuomba rushwa ya Sh. Milioni mbili.

Mbali na  Ngalawa, washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Askari Polisi wa kituo cha Polisi Osterbay, H  4810 PC Ramadhani Uweza (28) na H 48 86 PC Simon Sugu (26).

Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi , wakili  wa  serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),  Sophia Gura amedai kuwa Oktoba 29, 2016 huko Kimara Mwisho ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walishawishi rushwa ya Sh. Milioni mbili kutoka kwa mfanyabiashara wa Karikaoo jijini hapa, Ramadhani Ntunzwe , ili iwe kishawishi cha kuweza kuachia  mizigo ya mfanyabiashara huyo, kwa madai kuwa waliukamatwa kwa madai ya kufanya udanganyifu wa bidhaa alizonazo na hivyo kuathiri ukadiriaji wa kodi, kazi ambayo ni ya mwajiriwa wake.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamekana shtaka hilo na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambapo wametakiwa kuwa na mdhamini moja mwenye kitambulisho, atakayesaini bondi ya sh. Milioni tano.

Kwa mijibu wa upanda wa Mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na wako katika hatua za mwisho kukamilisha. Kesi imeahirishwa hadi Julai 10, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages